NA Eleuteri Mangi
Kikundi cha hamasa cha Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kimetia fora na kimegeuka kivutio wakati wa mechi ya Taifa Stars na Niger Juni 18, 2023 jijini Dar es salaam.
Hakika wameonesha na kudhihirisha uzalendo wa pekee wakishangilia kwa kupiga vuvuzela kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mchezo wakivalia jezi ya timu ya taifa lao ya rangi ya bluu ikiwa na picha nzuri ya mnyama Twiga.
Hii ni Wizara ya furaha na nguvu shawishi ya Taifa, ndiyo shina na burudani yao. Ndiyo maana wapo mstari wa mbele kuiambia Dunia wao hawatungi Sera, Sheria na Kanuni tu, bali wanafanya kazi ya Sanaa kudhihirisha umamju wao.
Hakika Viongozi, Hamad ni iliyopo kibindoni, hawa wamedhirishia umma wa Watanzani kuwa burudani ni jadi yao.
Hongera Waziri mwenye dhamana ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Pindi Chana, Naibu Waziri Mhe. Hamis Mwinjuma, Katibu Mkuu Bw. Saidi Yakubu na Naibu Katibu Mkuu wake Bw. Nicholas Mkapa, Kikundi cha hamasa cha Wizara, hongereni kwa kuitendea haki taaluma yenu Sanaa na Utamaduni.
Mwandishi wa makala haya anasema wapeni maua yao wanakikundi hiki wapatao 15 ili wawe chanzo cha buridani ya Watanzania wakati wote.