Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais anayesiamia Muungano Bw. Abdallah Mitawa akifungua kikao kazi kati ya ofisi hiyo na Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF kinachofanyika leo Jumatatu Juni 19,2023 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jijini Dar es Salaam, ambapo moja ya mambo yatakayojadiliwa katika kikoa hicho ni suala zima la uharibifu wa Mazingira, Mabadiliko ya tabia nchi na namna serikali kupitia ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira inavyoshuhulikia changamoto hiyo.
Bi Sara Kibonde Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira akitoa maelezo ya awali kabla ya kuaza kwa kikao kazi hicho kati ya ofisi hiyo na Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF kinachofanyika kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jijiniDar es Salaam.
Dkt. Andrew Komba MKurugenzi wa mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais akiwasilisha mada kuhusu mazingira wakati wa kikao kazi hicho kinachofanyika kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jijiniDar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kituo cha Ufuatiliaji wa Hewa Ukaa NCMC Profesa Eliakim Zahabu akiwasilisha mada Aina ya Miradi ya Kaboni wakati kikao kazi hicho kikiendelea kwenye Chuo Kikuu cha dar es Salaam jijini Dar es Salaamleo Jumatatu Juni 19,2023 huku wahariri hao wakifuatilia mada.
Bi Risper Koyi Mtaalam wa Masuala ya Kaboni Kitengo cha Huduma za Sheria Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira akiwasilisha mada ya sheria zinazosimamia mazingira katika kikao kazi hicho.
Baadhi ya Wahariri kutoka Jukwaa la wahariri TEF wakifuatilia uwasilishaji huo kutoka kwa Dkt. Andrew Komba
Picha ya pamoja.