Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo amewataka Wananchi wa Kata ya Handali,Wilaya ya Chamwino wasiwe kiwanda cha kuzalisha mabinti wa ndani na badala yake wawe kiwanda cha kuzalisha wataalamu Nchini.
Ameyasema hayo muda mfupi baada ya kushiriki kikao kwa Balozi wa Shina namba mbili katika tawi la Handali, Kata ya Handali.
Akizungumza na Wananchi pamoja na wana CCM Chongolo amewataka wazazi na walezi kuacha kuwafanyisha mabinti shughuli ambazo si zao na badala yao wawapeleke shule ila kupata ujuzi.
Amewaambia urithi ulio bora kwa watoto ni urithi wa Elimu hivyo kuwasomesha itawasaidia kuwalpeleka katika hatua ya maendeleo.
Katibu Mkuu huyo wa CCM bado yupo katika ziara ya kukagua Uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.
Ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Sophia Mjema pamoja na Katibu wa NEC Oganaizesheni Issa Haji Gavu ambapo wametembelea Wilaya ya Chamwino.