Waziri Wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI mh. Angellah Kairuki na Mwenyekiti Wa kamati ya Bunge la kudumu Tamisemi Mh.Denis Londo na wajumbe wa Kamati hiyo wakikagua miradimbalimbali ya DART inayotekelezwa na Shirika hilo wakati Wa Ziara iliyofanyika jijini Dar es salaam leo Juni 17,2023.
Waziri Wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Angellah Kairuki akmsikiliza Mwenyekiti Wa kamati ya Bunge ya Kudumu TAMISEMI Mh.Denis Londo wakati alipokuwa akizungumza na watumishi washirika hilo kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya DART Dkt. Florens Turuka.
………………………………..
Kamati ya Bunge ya Kudumu ya TAMISEMI imeishauri Serikali Kuandaa na Kutenga Maeneo Mapema yatakayotumika Kuongeza Miundombinu ili kukwepa kulipa Fidia pindi Watakapohitaji Kuendeleza miundombinu ya DART katika Miji mbalimbali nchini.
Hayo yameelezzwa na Mwenyekiti Wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya TAMISEMI Mh.Denis Londo kwa niaba ya wajumbe Wa kamati hiyo Mara Baada yakutembelea na kukagua miradi mbalimbali ambayo ujenzi Wa barabara za magari yaendayo Kwa haraka na vituo unaoendelea.
Kamati hiyo imepokea changamoto iliyobainishwa na Mtendaji Mkuu Wa DART kuwa wanakabiliwa na ugumu katika upatikanaji Wa maeneo wakati wanapohitaji kuongeza miundimbinu ya Mabasi yaendayo Kwa haraka ,Karakana, Vituo vya Mabasi na maeneo ya maegesho.
Mh Londo amesema kuna haja Serikali kuandaa maeneo ili kupunguza gharama ambazo zingetumika katika ulipaji fidia kwa wananchi badala yake ijipange Kwa ujenzi ambapo Serikali itakuwa imenufaika kwa kujengwa kwa gharama nafuu.
Aidha kamati hiyo pia imeishauri serikali kuweka utaratibu Wa kuwaendeleza watanzania wanaoshiriki katika ujenzi wa miradi kwa kuwapa vyeti kwa wale ambao wataonekana kufanya vizuri katika ushiriki wao wakazi.
Hii itawasaidia kupata ajira mahala pengine wakati mradi unapoisha, Sanjari na hayo Kamati hiyo meitaka Serikali kuhakikisha kwenye kila Mradi kuwepo na Mzawa mmoja atakayeweza kupata ujuzi Zaidi kwani itasaidia kupata wataalam wazawa wengi watakaoijua teknolojia kuhusu miradi hiyo .
Naye Waziri Wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI mh. Angellah Kairuki amesema anajivunia uwepo wa DART kwani wameweza kuendeleza na kutunza miundombinu vizuri na huku akiahidi kuandaa rasimu ya sheria mahsusi ya wakala Wa Mabasi yaendayo haraka itakayosaidia kutatua vikwazo katika utekelezaji Wa majukumu ya taasisi hiyo ili kuongeza pia huduma hiyo katika majiji mengie.
Ujenzi wa awamu ya tatu ambao unahusisha barabara ya Nyerere hadi Gongo la Mboto zenye urefu wa kilomita 23.6 unajengwa Kwa mgawanyo Wa mafungu Mawili ambapo kipande cha kwanza kinajengwa na mkandarasi Kampuni ya Sino Hydro kutoka China na Kwa upande Wa majengo mapitio ya usanifu yako katika hatua za mwisho na yatajengwa na kampuni ya UNITEC Civil Consultants Ltd ya Tanzania.