Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Mzumbe ya Ndaki ya Dar es Salaam Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Coretha Komba akimkabidhi Bi. Isabella Shitindi baadhi zawadi ikiwemo pipi na biskuti kwa ajili ya Watoto wa Mahabusu Upanga, Jijini Dar es Salaam katika kusherekea Siku ya Mtoto wa Afrika leo tarehe 16/6/2023.
Meneja wa Mahabusu ya Watoto, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Darius Kalijongo pamoja wageni waliotembelea Kituo Cha Watoto wa Mahabusu Upanga, Jijini Dar es Salaam wakifanya maombi maalamu kwa ajili ya kuwaombea aliyekuwa Rasi wa Ndaki ya Dar es Salaam Chuo Kikuu Mzumbe Marehemu Prof. Honest Ngowi na Dreva wake Inocent Mringo waliofariki wiki moja baada ya kutembelea Kituo hicho na kutoa msaada wa mahitaji kwa watoto wa Mahabusu.
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Mzumbe ya Ndaki ya Dar es Salaam Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Coretha Komba
Meneja wa Mahabusu ya Watoto, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Darius Kalijongo akishukuru baada ya kupokea zawadi za watoto kutoka Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam katika Siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika leo tarehe 16/6/2023 Kituoni hapo.
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Coretha Komba akitoa salaam za Chuo kwa niaba ya Rasi wa Ndaki wakati wa sherehe ya Mtoto wa Afrika zilizofanyika leo tarehe 16/6/2023 katika Mahabusu ya Watoto Upanga, jijini Dar es Salaam
……….
Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam leo tarehe 16 Juni 2023 wameadhimisha ya Siku ya Mtoto wa Afrika kwa kutoa zawadi katika Kituo cha Mahabusu ya Watoto Upanga kilichopo Jijini Dar es Salaam.
Siku ya Mtoto wa Afrika yamefikia kilele leo huku kauli mbiu ikiwa “Zingatia Usalama wa Watoto katika Ulimwengu wa Kidigitali”
Akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi Kituoni hapo, Kaimu Rasi wa Ndaki ya Dar es Salaam Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Coretha Komba, amesema kuwa Chuo Kikuu Mzumbe kimekuwa kikishirikiana na kituo hicho katika kuchangia mahitaji mbalimbali yanayohitajika kituoni hapo ikiwa ni sehemu ya kurudisha huduma kwa jamii pamoja na kuonyesha upendo kwa watoto hao.
Dkt. Komba amewahasa watoto hao kushika wanachofundishwa na walezi wao ili baadaye waweze kujiendeleza kielimu na wakipata nafasi wajiunge na Chuo Kikuu Mzumbe, kwani tuna ushirikiano wa muda mrefu.
“Leo watoto tumekuja kuwatembelea na kuwapa zawadi, tunawapenda na kuwajali ndio maana kila mwaka tunakuja kuwaona marafiki na majirani zetu, lakini mpo hapa kwa ajili ya kujifunza kwani mnafundishwa mambo mbalimbali na walezi wenu mshike sana mnachofundishwa ili baadaye mje kusoma Mzumbe.” alisisitiza Dkt. Coretha .
Chuo Kikuu Mzumbe kimekabidhi mahitaji mbalimbali zikiwemo pipi na biskuti ili kufanikisha sherehe ya siku ya Mtoto wa Afrika iliyoandaliwa kituoni hapo.
Kwa upande wake Meneja wa Mahabusu ya Watoto, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Darius Kalijongo, ameishukuru Chuo kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam kwa ushirikiano wanaowapatia katika kutoa mahitaji muhimu ya watoto.
“Chuo Kikuu Mzumbe ni miongoni wa taasisi tunazoshirikiana nazo kwa ukaribu na wamekuwa wakitusaidia pale tunapowaomba hitaji kwa ajili ya watoto wetu.” alisisitiza Bw. Kalijongo.
Hata hivyo Bw. Kalijongo aliwaomba walikwa wa sherehe hiyo kusimama kwa dakika mmoja ili kumkumbuka aliyekuwa Rasi wa Ndaki ya Dar es salaam Marehemu Prof. Honest Ngowi na dreva wake Innocent Mringo ambao waliyefariki wiki mmoja baada ya kuwatembelea kituo wakiwa na wafanyakazi wezake walipoleta mahitaji muhimu kwa watoto.