Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (wa pili kutoka kulia) akipiga makofi baada ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suruhu Hassani kuzindua rasmi Maadhimisho ya Miaka 25 ya Mafanikio ya Benki ya NMB.
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suruhu Hassani akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali katika hafla ya kuadhimisha miaka 25 ya Mafanikio ya Benki ya NMB yaliofanyika leo tarehe 17/6/2023 katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya Washiriki wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, wafanyakazi wa Benki ya NMB wakiwa katika hafla ya kuadhimisha miaka 25 ya Mafanikio ya Benki ya NMB yaliofanyika leo tarehe 17/6/2023 katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
……….
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Benki ya NMB imetenga Shilingi bilioni 2.5 kwa ajili ya kujenga Shule ya Mfano katika eneo na Mkoa ambao atapendekeza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suruhu Hassani.
Akizungumza katika hafla ya kuadhimisha miaka 25 ya Mafanikio ya Benki ya NMB yaliofanyika leo tarehe 17/6/2023 katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, amesema kuwa lengo la kujenga Shule ni kuhakikisha sekta ya elimu inapiga hatua na kupata mafanikio.
Amesema kuwa mafanikio ya Benki ya NMB yanapaswa kuendana jamii katika kuhakikisha wanatatua changamoto zilizopo.
Bi. Zaipuna amesema kuwa Benki ya NMB itaendelea kuwa mdau mkubwa wa uwekezaji nchini kupitia kilimo na biashara.
Amebainisha kuwa wamefanikiwa kutoa mikopo trilioni 5.2 kwa wakulima, wafanyabiashara biashara pamoja na watu binafsi.
“Mwaka huu tumefanya maboresha katika hospital ya Taifa ya Muhimbili katika hodi ya kujifungulia wakina mama kwa kununua vifaa mbalimbali pamoja na vitanda” amesema Bi. Zaipuna