Meneja wa Utafiti na Ubunifu Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Dkt. Daniel Komwihangilo akitoa matokeo ya utafiti katika sekta ya mifugo kuhusu mchango wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu leo tarehe 15/6/2023 katika Kongamano 8 la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STICE),
ambalo limeandaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) , limeingia siku pili, linalofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa Cha Mikutano Cha Kumbukumbu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam (PICHA NA JOHN BUKUKU)
Dkt. Simon Kangwe kutoka Kituo Cha Dar es Salaam Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) akitoa matokeo ya utafiti katika sekta Uvuvi kuhusu mchango wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu.
Baadhi ya Makatibu Wakuu ikiwemo Wizara ya Mifugo, Uvuvi, Fedha na Mipango wakisikiliza matokeo ya utafiti kuhusu mchango Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ulivyochangia kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali nchini.
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Sayansi, Teknolojia na Ubunifu imesaidia sekta ya mifugo kwa asilimia kubwa katika nyanja mbalimbali ikiwemo uzalisha malisho bora, utengenezaji wa vyakula kwa ajili ya mifugo pamoja na taasisi zinazozalisha chanjo na dawa.
Akizungumza leo tarehe 15/6/2023 Jijini Dar es Salaam wakati akitoa matokeo ya utafiti katika sekta ya mifugo kuhusu mchango wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu katika Kongamano 8 la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STICE),
ambalo limeandaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) , limeingia siku ya pili, Meneja wa Utafiti na Ubunifu Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Dkt. Daniel Komwihangilo, amesema kuwa pia katika matokeo hayo wameangalia mambo yaliofanyika katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2011 hadi 2021.
Dkt. Komwihangilo amesema kuwa kuna mambo mengi yamefanyika kupitia sayansi, teknolojia na ubunifu katika sekta ya mifugo na kuendelea kufanya vizuri katika mifugo ikiwemo Ng’ombe wa nyama na maziwa, mbuzi, kuku pamoja na mifugo mengine.
Amesema kuwa mchango wa sayansi, teknolojia na ubunifu katika sekta ya mifugo imeifanya kuwa kudhibiti katika Kuzuia magonjwa ya mifugo pamoja na kuzalisha mifugo bora.
“Wananchi wameendelea kufuga mifugo kisasa na kuleta tija katika kuongeza kipato chao, kuchangia katika upatikanaji wa chakula na ajira pamoja na upatikanaji wa mazao mbalimbali ya mifugo ikiwemo maziwa, nyama, ngozi” amesema Dkt. Komwihangilo
Amesema kuwa teknolojia imemsaidia mkulima kuingiza pato la Taifa pamoja na kuhakikisha usalama wa chakula unapatikana.
Amebainisha kuwa sasa hivi vijana wamekuwa na mwamko katika sekta ya unenepeshaji wa mifugo kupitia taasisi pamoja na idara mbalimbali.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Dodoma ( UDOM) Profesa Lughano Kusilika, amesema kuwa taifa linapaswa kuendelea kuhihimiza vijana kusoma sayansi ili kuleta tija.
Amesema kuwa tafiti zinaonyesha kwa nchi za Afrika ikiwemo Tanzania imekuwa ikienda kasi katika matumizi ya tehama.