Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Maghembe wakati alipofanya ziara kwenye Maabara Kuu ya Chakula na Lishe Mikocheni jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Juni 16, 2023 kukagua shughuli mbalimbali za maabara hiyo.
Dkt Germana Leyna Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania akitoa taarifa kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Maghembe wakati alipofanya ziara kwenye Maabara hiyo ili kuona shughuli mbalimbali zinaofanyika.
(PICHA NA JOHN BUKUKU)
……………………………………………
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) imetakiwa kutumia vizuri matokeo ya tafiti wanayofanya kwa kutumia lugha rafiki kuelimisha jamii katika nyanja mbalimbali ikiwemo namna bora ya kuifadhi, kuandaa pamoja na aina chakula wanachopaswa kutumia kulingana na mazingira.
Akizungumza wakati alipofanya ziara kwenye Maabara Kuu ya Chakula na Lishe Mikocheni jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Juni 16, 2023, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Maghembe, amesema kuwa ili Taifa lipige hatua kiuchumi linapaswa kuwa na watu wenye afya bora ambayo itawafanya wewe na nguvu ya kufanya kazi.
Dkt. Maghembe amesema kuwa ili kufikia malengo maafisa lishe wanatakiwa kutumia matokeo ya tafiti kuelimisha jamii kwa njia tafauti ili wawe na uwelewa mzuri katika lishe.
“Mwananchi anataka kujua atumie kiasi gani cha chakula, aina gani ?, pia watumie vipimo ambavyo anaweza kujua kwa haraka mfano kutumia chumvi kijiko kimoja au kunywa chai kikobe kimoja kwa siku, tutumia lugha rafiki kwao” amesema Dkt. Maghembe.
Amesema kuwa wakati umefika kwa taasisi ya lishe kuwa karibu na jamii katika kuwapa elimu jambo ambalo litasaidia kuleta tija kwa Taifa na kufikia malengo.
Dkt. Maghembe amefafanua bado kuna watu wengi hawana elimu ya lishe ikiwemo maeneo ya huduma za afya hospital ambapo kuna wagonjwa ambao wanaitaji kula aina fulani ya chakula ili wapone.
“Nendeni mkatoe elimu ya lishe katika Zanahati, vituo vya afya, hospital za Rufaa katika kliniki wamama wajawazito ” amesema Dkt. Maghembe.
Dkt Germana Leyna Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania akitoa taarifa kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Maghembe wakati alipofanya ziara kwenye Maabara hiyo ili kuona shughuli mbalimbali zinaofanyika.
Wafanyakazi mbalimbali wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Maghembe wakati alipofanya ziara kwenye Maabara hiyo ili kuona shughuli mbalimbali zinaofanyika.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Maghembe akisisitia jambo wakati alipozungumza na wafanyakazi kwenye Maabara Kuu ya Taasisi ya Chakula na Lishe ili kuona shughuli mbalimbali zinaofanyika kulia ni Dkt Germana Leyna Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania na kushoto ni [8:39 am, 16/06/2023] John Bukuku: Dkt. Analice Kamala Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi ya Chakula na lishe TFNC.
Picha mbalimbaliikimuonesha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Maghembe kulia wakati alipofanya ziara kwenye Maabara Kuu ya Chakula na Lishe Mikocheni jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Juni 16, 2023 kukagua shughuli mbalimbali za maabara hiyo katikati ni Dkt. Analice Kamala Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi ya Chakula na lishe TFNC na kushoto ni Dkt. Analice Kamala Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi ya Chakula na Lishe TFNC.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Maghembe akipata maelezo kutokakwa Tedson Lukindo msimamizi wa Maabara TFNC wakati alipofanya ziara kwenye Maabara Kuu ya Chakula na Lishe Mikocheni jijini Dar es Salaam.