Geneva, Uswiss: Tarehe 2/06/2023.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Dkt. Ladislaus Chang’a, ameongoza Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano Mkuu wa kumi na tisa wa WMO uliofanyika Geneva, Uswiss kuanzia tarehe 22 Mei hadi 2 Juni, 2023.
Sambamba na masuala mengine, mkutano huo ulipitisha vipaumbele vikuu vitatu vya kimkakati vya masuala ya hali ya hewa katika kipindi cha mwaka 2024 hadi 2027. Miongoni mwa vipaumbele hivyo, kipaumbele kikuu ni utekelezaji wa programu ya Umoja wa Mataifa ya “Taarifa za tahadhari za mapema kwa wote (Early Warning for All – EW4All)”, ambayo lengo lake ni kupunguza majanga yanayosababishwa na hali mbaya ya hewa kwa kuwezesha kila mtu kupata taarifa za hali ya hewa ifikapo mwaka 2027. Nchi wanachama zimeaswa kuandaa mikakati ya kutekeleza EW4All na kuandaa taarifa za utekelezaji wa programu hiyo. Maeneo mengine ya kipaumbele yaliyopitishwa ni Uimarishaji wa uangazi na ubadilishanaji wa data za hali ya hewa ili kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi Sambamba na vipaumbele hivyo, mkutano wa congress wa 19 ulipitisha mpango mkakati wa WMO utakaotekelezwa katika kipindi cha 2024-2027 ambao una malengo matano (5).
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo ukiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika WMO, Dkt. Ladislaus Chang’a, ulishiriki kikamilifu na kuchangia katika masuala yaliyoafikiwa kwa manufaa ya nchi yetu na Afrika. Miongoni mwa masuala ambayo Tanzania ilichangia ni programu ya Kuimarisha Uangazi “Systematic Observation Financing Facility (SOFF)” inayotekelezwa katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania kwa lengo la kusaidia kuboresha uangazi ili kuwezesha upatikanaji na ubadilishanaji wa data wa hali ya hewa kwa nchi zinazoendelea. Akichangia kuhusiana na utekelezaji wa programu ya SOFF nchini Tanzania, Dkt. Ladislaus Chang’a alishauri WMO.