Naibu Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Antony Mavunde (katikati) alifanya usafi wa kusafisha mtaro wa maji katika eneo la Makole, Manispaa ya Dodoma leo Ijumaa (Juni 2, 2023) ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za Wiki ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani inayotarajia kuadhimishwa duniani kote ifikapo Juni 5 mwaka huu. Wa pili kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Switbert Mkama.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Switbert Mkama akifanya usafi wa kusafisha mtaro wa maji katika eneo la Makore Manispaa ya Dodoma leo Ijumaa Juni 2, 2023 ) ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za Wiki ya Maadhimisho ya Siku ya
Mazingira Duniani inayotarajia kuadhimishwa duniani kote ifikapo Juni 5 mwaka huu.
Naibu Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Antony Mavunde pamoja na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Godwin Gondwe wakifanya usafi wa
mazingira katika eneo la Makole, Manispaa ya Dodoma leo Ijumaa (Juni 2, 2023) ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za Wiki ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani inayotarajia kuadhimishwa duniani kote ifikapo Juni 5 mwaka huu. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Switbert Mkama.
Naibu Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Dodoma Mjini, Mhe. Antony Mavunde
akiongozana na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma , Mhe. Godwin Gondwe wakati wa zoezi la usafi wa mazingira katika eneo la Makole, Manispaa ya Dodoma leo Ijumaa (Juni 2, 2023) ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za Wiki ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani inayotarajia kuadhimishwa duniani kote ifikapo Juni 5 mwaka huu. Nyuma ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Switbert Mkama.
Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma, Bi. Fatma Mganga akitoa salamu za ukaribisho kwa Naibu Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Dodoma Mjini, Mhe. Antony Maunde wakati wa wakati wa zoezi la usafi wa mazingira katika eneo la Makole, Manispaa ya Dodoma leo Ijumaa (Juni 2, 2023) ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za Wiki ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani inayotarajia kuadhimishwa duniani kote ifikapo Juni 5 mwaka huu. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Switbert Mkama.
Naibu Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Dodoma Mjini, Mhe. Antony Mavunde
akibadilishana mawazo na Viongozi na wananchi mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa zoezi la usafi wa mazingira katik eneo la katika eneo la Makole, Manispaa ya Dodoma leo Ijumaa (Juni 2, 2023) ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za Wiki ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani inayotarajia kuadhimishwa duniani kote ifikapo Juni 5 mwaka huu. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Switbert Mkama.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Switbert Mkama (kulia)akibadilishana mawazo na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Godwin Godwe mara baada ya kumalizika kwa zoezi la usafi wa mazingira katik eneo la katika eneo la Makole, Manispaa ya Dodoma leo Ijumaa (Juni 2, 2023) ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za Wiki ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani inayotarajia kuadhimishwa duniani kote ifikapo Juni 5 mwaka huu.
………………………………………
SERIKALI imewakemea wafanyabiashara wachache wasio waaminifu wanaoendelea
kuingiza, kuzalisha na kusambaza bidhaa za plastiki zisizokidhi viwango zinazotumika kama vifungashio ambavyo zimekuwa chachu ya uchafuzi wa mazingira katika maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumza katika zoezi la usafi wa mazingira katika kuelekea kilele cha Siku ya
Mazingira Duniani Juni 5 mwaka huu leo Ijumaa (Juni 2, 2023) Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Antony Mavunde amesema ni wajibu wa Wafanyabiashara kushirikiana na taasisi za Serikali katika kusimamia usitishaji wa Matumizi ya bidhaa za plastiki.
“Kumekuwa na juhudi mbalimbali za Serikali na wadau katika kukabiliana na uchafuzi wa mazingira utokanao na taka za plastiki, hata hivyo bado kuna ukwiukwaji wa sharia kwa baadhi ya wafanyabiashara wanaoingia na kuzalisha mifuko ya plastiki isiyokidhi viwango ambayo inayotumika madukani na watoa huduma” amesema Mhe. Mavunde. Kwa mujibu wa Mavunde amewaka wananchi kuendelea kuiunga mkono Serikali katika kudhibiti matumizi ya mifuko na bidhaa za plastiki kwa kutoa ushirikiano kwa viongozi wa serikali za mitaaa ili kkurahisisha zoezi hilo la kutokomeza vifungashio visivyokidhi viwango ambavyo vimekuwa visambazwa kupitia njia za panya.
Aidha Mavunde amesema Serikali kupitia Ofisi ya Makamu imeendelea kufanya jitihada kubwa za kuhamasisha suala la utunzaji na uhifadhi wa mazingira katika maeneo ya miji mikuu nchini ikiwemo Jiji la Dodoma, hivyo ni wajibu wa wananchi kuwataka wakazi wa Dodoma na Tanzania kwa ujumla kutosubiri Kilele cha Maadhimisho ya mazingira katika kujishughulisha na suala la usafi katika maeneo yao.
Katika hatua nyingine, Mavunde amewataka wananchi kujenga utamaduni wa kufanya usafi na kuwa sehemu ya maisha yao ya kila siku kwa kuhakikisha maeneo yao yanakuwa safi na salama kwa ajili ya ustawi na maendeleo yao ya kijamii na kiuchumi.
Awali akimkaribisha Mgeni rasmi, Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Switbert Mkama amesema katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya
Mazingira Duniani, Ofisi hiyo imejipanga kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma hatua inayolenga kupendezesha taswira ya Jiji hilo ambalo ni makao makuu ya Serikali.
Kuanzia jana Juni Mosi ambayo tulizindua Wiki ya Mazingira tumeanza kwa kufanya
usafi wa mazingira na kupanda miti katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma. Zoezi hili litaendelea hadi siku ya Kilele Siku ya Jumatatu Juni 5 mwaka huu” amesema Dkt. Mkama.
Akitoa salamu za Mkoa wa Dodoma, Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Godwin Gondwe
ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amesema Mkoa huo itaendelea
kuunga mkono juhudi za Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuhakikisha
kuwa Jiji la Dodoma ambalo ni Makao Makuu ya Serikali linaendelea kuwa safi.
Kilele cha Wiki ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo ina kauli mbiu
isemayo Pinga Uchafuzi wa Mazingira unaotokana na Taka za Plastiki inatarajia
kuwa Juni 5 mwaka huu, ambapo Mgeni rasmi anatarajia kuwa Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango.