Angela Msimbira TABORA
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Mchezo Mhe. Hamis Mwinjuma ametoa wito kwa wadau wa michezo nchini kuunga mkono juhudi za serikali katika kuendeleza sekta ya michezo kwa kuwekeza katika vituo vya michezo, miundombinu ya michezo na kufungua akademia za michezo ili kukuza na kuendeleza vipaji.
Akifungua Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa wanafunzi wa shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) leo Juni 15, 2023 Mkoani Tabora.
“Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameonyesha dhamira ya dhati ya kuendeleza michezo nchini kwa kuruhusu na kuwezesha kufanyika kwa mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA, Rais wetu ni mwanamichezo, wote ni mashahidi wa jitihada zote kuboresha sekta ya michezo nchini”amesema
Mhe. Mwinjuma amesema msingi wa mafanikio ya michezo nchini huanzia katika ngazi ya msingi hivyo ni vyema wadau wakawekeza ili kupata vipaji vya wananichezo nchini
Ameendelea kufafanua kuwa mashindano haya yanalenga katika kuibua na kuendeleza vipaji vya wanamichezo chipukizi ambao wanapatikana katika mashindano haya.
Aidha, Mhe. Mwinjuma amesema uwepo wa mashindano ya michezo kuanzia ngazi ya msingi huleta chachu ya kufikia mafanikio zaidi katika sekta ya michezo nchini.
Kadhalika, amewaagiza Maafisa Elimu wa mikoa yote nchini kuhakikisha kuwa wanazisimamia vema shule teule za michezo zilizo katika maeneo yao.
Amesema Serikali inaendelea kukarabati miundombinu ya Michezo katika shule Teule 56 za Michezo Nchini za Sekondari zinahusisha shule mbili kwa kila Mkoa, kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA Taifa Bw. George Mbijima amesema jumla ya wanafunzi 3,171 ikijimuisha wasichana 1571 na wavulana 1,600