Na Victor Masangu, Kibaha
Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Selina Koka ameahidi kushirikiana bega kwa bega na jumuiya ya wazazi kwa lengo la kuwawezesha kiuchumi katika nyanja mbali mbali ili kuleta chachu ya maendeleo.
Selina ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya jumuiya ya wazazi Mkoa wa Pwani amebainiisha kuwa lengo lake kubwa ni kuendelea kufanya kazi kwa pamoja katika ngazi zote lengo ikiwa ni kuiimarisha jumuiya hiyo.
Aliyasema hayo wakati wa mkutano wa kuhitimisha ziara ya jumuiya ya wazazi Wilaya ya Kibaha mjini ambapo ilifanyika katika kata ya kongowe na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa chama pamoja na jjumuiya zake.
“Napenda kusema kwamba nitaendelea kushirikiana na nyinyi katika suala zima la kuweka misingi imara ya jumuiya hii ya wazazi inasonga mbele zaidi katika suala zima la kiuchumi na mimi nitaendelea kushirikiana katika kila nyanna,”alisema Selina Koka.
Kadhalika aliwapongeza viongozi wa jumuiya hiyo ya wazazi Wilaya ya Kibaha mjini kwa kumaliza ziara katika kata zote 14 za Jimbo la Kibaha mjini ambayo imeweza kuleta tija zaidi katika kuimarisha jumuiya kuanzia ngazi za chini.
“Nimefarijika kujumuika na nyinyi katika siku ya leo na wana chama wa CCM hasa jumuiya hii ya wazazi na kwamba mheshimiwa Mbunge anawasalimu Sana kwani kwa sasa yupo katika vikao vya bunge lakini yupo pamoja nanyi katika kuleta maendeleo.
Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Kibaha mjini imehitimisha ziara yake katika kata ya kongowe ambapo imeweza kutembelea kata zote 14 za Jimbo la Kibaha mjini kwa ajili ya kuzungumza na wanachama kuangalia uhai wa chama na kutoa shukrani kwa wanachama.