Na WAF, Bungeni Dodoma
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amebainisha kuwa, tafiti zinaonesha hali ya umanjano ikitokea kwa mtoto mchanga ndani ya saa 24 baada ya kuzaliwa inaonesha tatizo la kiafya (Pathological ) na tiba stahiki linahitajika baada ya kutambua tatizo hilo.
Dkt. Mollel amesema hayo leo Juni 15, 2023 wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu Mhe. Lucy John Sabu, Bungeni Jijini Dodoma.
Amesema, tatizo hili likitokea baada ya masaa 24, mara nyingi linatokana na sababu za kawaida za mwili wa mtoto kupunguza chembechembe nyekundu nyingi alizokuwa nazo tumboni kwa Mama, hata hivyo hili pia uchunguzi wa kina ni muhimu ili kujihakikishia.