Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na ujumbe wa Shirika la Danish Refugee Council ukiongozwa na Meneja Bi. Jo Povey (kushoto) na Bw. Alfred Magehema waliomtembelea jijini Dodoma leo Juni 14, 2023 kwa lengo la kuwasilisha mpango wa shughuli za kuhifadhi mazingira.
……
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amepongeza wadau kwa juhudi za kuhifadhi mazingira na kuonesha nia ya kufanya Biashara ya Kaboni nchini.
Amesema hayo alipokutana na Meneja wa Shirika linalohudumia wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) la Denmark Bi. Jo Povey katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma leo Juni 14, 2023.
Dkt. Jafo amesema Serikali inatambua juhudi za wadau hao ambao wanafanya shughuli za kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti katika kambi za wakimbizi zilizopo mkoani Kigoma na wananchi wanaozunguka kambi hizo.
Amesema kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Raia sasa inaendelea kuzifanyia kazi Kanuni na Mwongozo wa Biashara ya Kaboni ili wananchi wanufaike na biashara hiyo.
Waziri Jafo amesema changamoto ya ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa ni ni kubwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini hali inayochangia uharibifu wa mazingira na ukame na kusababisha upungufu wa maji na chakula.
Hivyo, amewashukuru wadau hao kwa kuonesha nia ya kuwekeza katika nishati mbadala ambayo kwa kiasi kikubwa itasaidia kupunguza kasi ya ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa.
“Tunafurahi tunapoona wadau kama ninyi mnashiriki kikamilifu katika kulinda mazingira na tunaona juhudi zenu zE kupanda miti, kutuletea nishati mbadala na kuona namna ya kusaidia katika uwekezaji wa hewa ya ukaa na kwqa upande wetu kama Serikali tunaendelea kuhamisha wananchi wahifadhi mazingira,“ amesema.
Kwa upande wake Meneja wa shirika hilo Bi. Jo amesema kipaumbele chao tangu mwaka 2021 ni kushirikiana na Serikali katika suala la upandaji wa miti ili kuhifadhi mazingira.
Amesema kwa kushirikiana na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) pamoja na Halmashauri ya Kibondo mkoani Kigoma wanapanda miti katika kambi za wakimbizi na maeneo ya jirani ili kurudisha hali ya mazingira iliyokuwepo awali.
“Kukiwa na mkusanyiko wa watu hususan wakimbizi wakikaa katika eneo moja lazima wawe na mahitaji kama ya kupikia na lazima wakate miti kwa ajili ya kuni kwa hiyo ni lazima kupanda tena miti, hivyo tumeona tufanye uhifadhi,“ amesema Bi. JoNaye
Meneja wa masuala ya uchumi wa shiriki hilo Bw. Alfred Magehema amesema kuwa kwa sasa wanatekelekeza mradi wa mkaa mbadala ambao unasambazwa katika kambi za wakimbizi.
Amesema katika kambi ya Nduta zinazalilishwa tani zaidi ya mbili kwa siku ambazo zinasaidia matumizi ya kila siku ya wakimbizi hivyo kusaidia kupunguza ukataji ovyo wa miti.
Pia, amepongeza Serikali ya Tanzania kwa kulipa uzito suala la Biashara ya Kaboni hatua ambayo inasaidia kupunguza uharibifu wa mazingira huku akisema shirika linatoa hamasa ya kuhifadhi misitu.