Msemaji wa Idara ya Masoko na Mipango Chuo Cha Furahika Bw. Siasa Digaga akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Cha Furahika kilichopo Buguruni Malapa, Jijini Dar es Salaam wakiwa darasani.
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Chuo Cha Furahika kilichopo Buguruni Malapa kupitia wadau ambao ni Wamishenary kutoka nchini Ujerumani wametenga Shilingi milioni 120 kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wanatakao jiunga na Chuo hicho kusoma kozi mbalimbali bila bure.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Idara ya Masoko na Mipango ya Chuo Cha Furahika Bw. Siasa Digaga, amesema kuwa Chuo Cha Furahika ni sehemu ya mradi wa kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suruhu Hassani katika kuhakikisha wanawasaidia vijana wanaotoka katika kaya maskini.
Bw. Digaga amesema kuwa mpaka sasa tayari wadau wametoa fedha Shillingi milioni 120 ili kuhakikisha vijana wanaotoka katika kaya maskini wanasoma fani ambayo itakwenda kumsaidia kujikwamua kiuchumi.
“Chuo cha Furahika kipo kwa ajili ya kuwezesha vijana kupata elimu ya kozi mbalimbali hasa waliomaliza elimu ya msingi na kidato cha nne na kushindwa kuendelea na masomo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo changamoto ya fedha” amesema Bw. Digaga.
Amesema kuwa Chuo kinaaza kupokea mwanafunzi kuanzia tarehe 16/6/2023 hadi tarehe 1/7/2023 kwa ajili ya kusoma kozi mbalimbali ikiwemo ushonaji, mapambo, udereva, secretary, ufundi magari, uuguzi, Computer, kiingereza, kifaransa pamoja hotel.
Amesema kuwa wakati umefika watanzania kuchangamkia fursa ya kusoma kozi bila kulipa ada.
“Mwanafunzi atachangia Shilingi 50,000 kwa ajili ya kununua vifaa vya kujifunzia kwa vitendo akiwa darasani, na gharama ya fomu kwa ajili ya kujiunga na chuo Shilingi 10,000” amesema Bw. Digaga.
Bw. Digaga amefafanua kuwa baada ya kulipia fedha kwa ajili ya kununua vifaa vya kujifunzia kwa vitendo pamoja na fomu ya kujiunga na chuo, mwanafunzi hatatoa fedha yoyote mpaka anamaliza masomo yake.
Ameeleza kuwa Chuo kina utaratibu wa kuwatafutia kazi wanafunzi baada ya kumaliza masomo yao.
“Tunatoa elimu bure kwa ajili ya kuwasaidia vijana ili wasijiunge na makundi mabaya ikiwemo kutumia dawa za kulevya, wizi pamoja na kushiriki ngono zembe” amesema Bw. Digaga.
Chuo kinakaribisha wanafunzi kusoma bure, lengo ni kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hasan ya Elimu bure, hivyo mashirika na watu mbali mbali wanakaribishwa kuleta wanafunzi na taasisi ama mashirika yenye namna ya kusaidia taasisi yetu wanakaribishwa pia, ili kuwanuia watoto wa kike kupata elimu iliyo bora.
Kwa taarifa zaidi kuhusu Chuo Cha Furahika unaweza kutekeleza website ya chuo kwa kubofya : https://www.furahikaeducation.com/