Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Utamaduni na Makumbusho ya Wasukuma Bujora, Magu Mkoani Mwanza tarehe 13 Juni, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akisaini Kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Utamaduni na Makumbusho ya Wasukuma Bujora, Magu Mkoani Mwanza tarehe 13 Juni, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akimsikiliza Askofu Mkuu Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza Renatus Nkwande kuhusu Kituo cha Utamaduni na Makumbusho ya Wasukuma Bujora mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Utamaduni na Makumbusho ya Wasukuma Bujora, Magu Mkoani Mwanza tarehe 13 Juni, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akimsikiliza Ndugu Richard Raphael Bulluma Mhifadhi wa Makumbusho ya Wasukuma Bujora kuhusu masuala mbalimbali ya Kabila la Wasukuma na maeneo waliokuwa wakiishi pamoja na shughuli mbalimbali walizokuwa wakizifanya wakati akitembelea Kituo cha Utamaduni na Makumbusho ya Wasukuma Bujora, Magu Mkoani Mwanza tarehe 13 Juni, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu na akiwa amekaa kwenye kiti cha Kifalme cha Watemi wa Kisukuma katika Kituo cha Utamaduni na Makumbusho ya Wasukuma Bujora, Magu Mkoani Mwanza tarehe 13 Juni, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akiwa pamoja na Machifu wenzake wakiangalia ngoma za Utamaduni wa Kisukuma (hazionekani pichani)wakati alipotembelea Kituo cha Utamaduni na Makumbusho ya Wasukuma Bujora, Magu Mkoani Mwanza tarehe 13 Juni, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akiwa pamoja na Machifu wenzake wakiangalia ngoma za Utamaduni wa Kisukuma (hazionekani pichani)wakati alipotembelea Kituo cha Utamaduni na Makumbusho ya Wasukuma Bujora, Magu Mkoani Mwanza tarehe 13 Juni, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akitembelea Kituo cha Utamaduni na Makumbusho ya Wasukuma Bujora, Magu Mkoani Mwanza tarehe 13 Juni, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akizungumza na Machifu mara baada ya kutembelea Kituo cha Utamaduni na Makumbusho ya Wasukuma Bujora, Magu Mkoani Mwanza tarehe 13 Juni, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akiwasalimia viongozi mbalimbali wakati akiwasili katika viwanja vya Red Cross, Ngomeni Kisesa kwa ajili ya kushiriki Tamasha la Bulabo, Magu Mkoani Mwanza tarehe 13 Juni, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akiwasili katika viwanja vya Red Cross, Ngomeni Kisesa kwa ajili ya kushiriki Tamasha la Bulabo, Magu Mkoani Mwanza tarehe 13 Juni, 2023
……
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imepanga kununua chakula na kuweka akiba katika maghala kwa kiasi cha tani laki tano kwa mwaka huu ikilinganishwa na tani laki mbili na hamsini kwa mwaka uliopita.
Rais Samia ameyasema hayo leo katika Tamasha la Utamaduni la Bulabo ambalo ni sherehe za kumshukuru Mungu kwa mavuno lililofanyika katika uwanja wa Red Cross Ngomeni uliopo Kisesa.
Aidha, Rais Samia amesema Serikali itajenga maghala ya chakula katika kila mkoa ili kuweza kuhifadhi chakula kitakachoweza kuhudumia wananchi katika kila mkoa.
Rais Samia pia amesema Serikali imejipanga kuhakikisha nchi inakuwa na chakula cha kutosha kwa kuongeza matumizi katika sekta ya chakula ikiwemo kuongeza fedha kwenye bajeti ya kilimo ili wananchi waweze kuzalisha ziada ya chakula.
Vile vile, Rais Samia amesema Serikali imetenga fedha kwa ajili ya kujenga skimu za umwagiliaji ili wakulima walime na kuvuna mara mbili kwa mwaka badala ya kutegemea mvua.
Kwa upande mwingine, Rais Samia amewataka Machifu kuhamasisha wananchi kufanya kazi na kuchangia katika shughuli za maendeleo ili kujenga taifa bora.
Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu