Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania Mh. Kassim Majaliwa akiwasili kwenye ukumbi wa Julius Nyerere JNICC jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuongoza kongamano la Viongozi mbali mbali wa kidini Leo Jumatatu 12,2023 wanaokutana kwa ajili ya mjadala wa kitaifa na kujengewa uelewa juu ya athari za sauti zilizozidi viwango katika nyumba ya ibada.
Kongamano hili limeandaliwa na Jumuiya ya Maridhiano Tanzania JMAT na NEMC kwa lengo la kutoa elimu juu ya suala Zima la athari za sauti zilizozidi viwango katika nyumba za ibada .
Pamoja na Mambo mbali mbali mada tisa zitawasilishwa kwenye kongamano hilo ili kujadiliwa na kufikia hatua zitakazosaidia kupunguzwa kwa kelele hizo katika nyumba za ibada.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania Mh. Kassim Majaliwa akiwa amesimama pamoja na viongozi kadhaa kwenye ukumbi wa Julius Nyerere JNICC jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuongoza kongamano la Viongozi mbali mbali wa kidini Leo wanaokutana katika kwa ajili ya Kongomano la kitaifa la kujengewa uelewa juu ya athari za sauti zilizozidi viwango katika nyumba za ibada kutoka kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Yusuf Hamad Masauni Waziri wa Mambo ya Ndani na katikati ni Balozi wa Mazingira Alhaj Alhadi Mussa Salum.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania Mh. Kassim Majaliwa akiwa amesimama pamoja na viongozi kadhaa kwenye ukumbi wa Julius Nyerere JNICC jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuongoza kongamano la Viongozi mbali mbali wa kidini Leo wanaokutana katika kwa ajili ya Kongomano la kitaifa la kujengewa uelewa juu ya athari za sauti zilizozidi viwango katika nyumba za ibada, kulia ni Dkt. Suleiman Jafo Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na kushoto ni Balozi wa Mazingira Alhaj Alhadi Mussa Salum.
Picha zkionesha viongozimbalimbali wa dini wakiwa katika kongamano hilo tayari kwa kumsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa wakatiatakapozungumza nao na baadaye kushiriki katika mjadala huo.