Kamishina Wa elimu Dkt Lyabwene Mtahabwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi kongamano hilo.
Mkurugenzi Mtendaji Wa Montessori Bi Sarah Kateleja
…………………….
Na Stamil Mohamed
Wazazi na walezi nchini wametakiwa kuwakuza watoto kwa misingi imara ya kimwili na akili kutengeneza Taifa bora.
Maagizo Hayo yametolewa Leo ,na Kamishina wa Elimu nchini Dkt Lyabwene Mtahabwa wakati wa kongamano la 26 la wa Montessori lililofanyika Katika ukumbi WA Msimbazi Center jijini Dar es salaam ambapo amewataka wazazi na walezi kutokuwaachia walimu pekee katika elimu ya awali na msingi ambayo ndio huanza kumjenga mtoto kiakili na Mwili .
Aidha amewaasa wazazi kuwa licha ya kuwapeleka shule watoto kupata elimu pia wawape wasaaa wa kujifunza maisha halisi ya kitanzania yatakayo wasaidia watoto uwelewa wa kutosha kuhusu Jamii Yao kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo nchini.
Hata hivyo katika kongamano hilo Mkurugenzi Mtendaji Wa Montessori Sarah Kiteleja amesema lengo la kongamano hilo ambalo hufanyika kila mwaka ni kuwajengea uwezo walezi wa vituo vya watoto na walimu,kukumbushana na kutathimini nini kifanyike kukuza watoto katika misingi iliyo imara ya tabia na akili ili kuwajengea watoto uwezo kuchanganua maswala mbalimbali Katika mazingira ya maisha ya Kila siku na makuzi Yao Kwa jumla.