Kaimu Mkurugenzi wa Makampuni na Majina ya Biashara Bw. Meinrad Rweyemamu akitoa mada kwa wahariri wa vyombo vya habari kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF katika kikao kazi kilichofanyika leo Juni 8,2023 kwenye ukumbi wa Julius Nyerere JNICC jijini
Dar es Salaam.
…………………………..
NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM.
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imetoa elimu kwa Wahariri wa vyombo vya habari nchini kuhusu huduma mbalimbali wanazotoa ikiwemo
umiliki wa manufaa katika kampuni jambo ambalo litawasaidia kufanya kazi kwa ufanisi katika kuelimisha umma.
Akizungumza leo tarehe 8/6/2023 Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Makampuni na Majina ya Biashara Bw. Meinrad Rweyemamu, amesema kuwa lengo la kukutana wahariri wa vyombo vya habari ni kujadili majukumu ya Brela pamoja na kuongeza ushirikiano katika utendaji.
Bw. Rweyemamu amesema kuwa vyombo vya habari ni muhimu katika kuelimisha umma ikiwemo wadau pamoja na huduma zinazotolewa na Brela.
“Wamepata elimu kuhusu kampuni, umiliki wa kampuni, nani anapaswa kuulizwa linapofanyika kosa na nani anapaswa kujibu ” amesema Bw. Rweyemamu.
Bi. Roida Andusamile MKuu wakitengo cha Maasliano Serikalini kutoka BRELA akifafanua jambo katika kikao kazi kati ya BRELA na Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF kilichofanyika kwenye ukumbi wa Julius Nyerere JNICC jijini Dar es Salaam leo Juni 8,2023.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Bw. Deodatus Balile akifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye kikaokazi hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Julis Nyerere JNICC jijini Dar es Salaam.
Picha zikionesha wahariri mbalimali wakiwa katika kikao kazi hicho.