Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na masoko wa AzamPesa Tanzania Gillian Rugumamu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Huduma ya kifedha ya AzamPesa iliyozindiliwa Kwenye ofisi za kampuni hiyo Masaki jijini Dar es Salaam Juni 6,2023.
Rehema Salim Meneja Uhusiano wa makampuni ya Bakhresa Group akifafanua jambo Katika uzinduzi wa Huduma hiyo ya AzamPesa iliyozinduliwa Leo Masaki jijini Dar es Salaam.
Rehema Salim Meneja Uhusiano wa makampuni ya Bakhresa Group Kushoto na Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na masoko wa AzamPesa Tanzania Gillian Rugumamu wakijadiliana jambo wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi.
Rehema Salim Meneja Uhusiano wa makampuni ya Bakhresa Group Kushoto na Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na masoko wa AzamPesa Tanzania Gillian Rugumamu wakiwa wameshika vibango vinavyoelekeza namna Huduma hiyo inavyofanya kazi wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi.
Usajili wa Huduma hiyo ikiendelea wakati wa uzinduzi.
…………………………..
Kampuni ya huduma za kifedha kupitia Simu ya Mkononi ya AzamPesa Money leo imezindua Promosheni yake mpya kwa wateja wote wanaotumia huduma ya kutuma na kupokea pesa kupitia AzamPesa ambapo wateja wote wataweza kutuma Pesa Bila Makato yeyote.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na masoko wa AzamPesa Tanzania Gillian Rugumamu amesema Huduma hii inayojulikana kama KUWA HURU – TUMA PESA BURE itawawezesha wateja wetu zaidi ya milioni 10 nchini kutuma na kupokea Pesa BURE” ambapo mfumo unaruhusu wateja kutoka mitandao yote ya simu kujiunga na kutumia huduma ya AzamPesa kwa watu wote wenye namba au simu za mkononi bila kubagua na kwa kiwango chochote.
KUWA HURU TUMA PESA BURE imekuja baada ya kuzingatia sana mahitaji ya wateja na tuna Imani kuwa promosheni hii itakuwa ni chachu kwa wale ambao sio wateja wa AzamPesa kuanza kutumia huduma hii salama, rahisi na ya uhakika. Tunatarajia kuona watanzania wote wakichangamkia Fursa hii ya kuishi maisha bila makato. Wateja wanaotumia huduma hii wataokoa kiasi cha pesa hadi Sh 5,400 kuanzia sasa” amesema Rugumamu
Rugumamu aliongeza kuwa “AzamPesa tumejiwekea mikakati ya kuendeleza huduma bora nchini kote na tumejikita Zaidi katika kuongeza Mawakala wetu nchi nzima. Tunaendelea kuongeza mawakala na kufanya huduma hii iwe rahisi Zaidi, sasa wakala anaweza kusajiliwa kuwa wakala wa AzamPesa kupitia chatbot yetu ya AzamPesa, +25560900000000. Atajisajili mwenyewe na huduma za Azampesa, kisha atatuma taarifa zake zilizohakikiwa na kugongwa muhuri na mwana sheria na sisi kupitia kitengo chetu tutapokea nyaraka zake na kumsajili haraka . Mawakala wetu hawatahitaji tena kusubiri sana wanaweza kujisajili na huduma hii popote pale walipo.
Pia wateja wetu watapata huduma ya AzamPesa kwa kupigia *150*08# au kutumia application ya AzamPesa kwa wateja wote walio na Simu Jana na kuanza kufurahia maisha haya.
Vilele AzamPesa Money inawezesha malipo mbalimbali yakiwemo yale ya huduma za serikali ( e-government) ambayo wateja wanaweza kufanya hayo malipo popote kwa wakati mmoja. “Pia huduma ya AzamPesa Money imeunganishwa na mabenki mbalimbali nchini ili kurahisha wateja kufanya miamala mbali mbali.