Muonekano wa gari walilokua wakisafiria Toyota Coaster yenye namba za usajili T .938 DVQ Lilikua linatokea Mkoani Mbeya Kuelekea Dear salam kugongana na Lori la Mzigo lenye namba za usajili T. 693 DMF katika eneo la Iyovi wilaya ya Kilosa Barabara kuu ya Morogoro _Iringa.
Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya St Kizito Mikumi Dokta Steven Mbilinyi akizungumza na waandishi wa habari.
Na Farida Mangube, Morogoro
Watu watano wamefariki na wengine 20 kujeruhiwa baada ya gari walilokua wakisafiria Toyota Coaster yenye namba za usajili T .938 DVQ Lilikua linatokea Mkoani Mbeya Kuelekea Dear salam kugongana na Lori la Mzigo lenye namba za usajili T. 693 DMF katika eneo la Iyovi wilaya ya Kilosa Barabara kuu ya Morogoro _Iringa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Alex Mkama amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Coaster ambaye jila lake halijafahamika kwa kutaka kuyapita magari yaliyopo mbele yake bila kuchukua tahadhari
Kwa Upande wake Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya St Kizito Mikumi Dokta Steven Mbilinyi amekili kupokea kwa miili ya watu watano waliopoteza maisha katika ajali hiyo.
“Tumepokea miili ya watu 5, wanaume 3 na wanawake 2 na majeruhi 20 kati yao 10 wametibiwa na tumewaruhusu na 9 wanaendelea kupatiwa matibabu na mmoja amepelekwa hospitali ya Rufaa mkoa Morogoro kwa matibabu zaidi.” Alisema Mganga Mfawidhi.