Waziri wa ujenzi mawasiliano na uchukuzi dkt. Khalid Salum Mohammed akiteta jambo na Waziri wa maendeleo ya jamii ,Jinsia wazee na watoto Riziki Pembe Juma katika mbio za mwenge huko kinyasini Wilaya ya Kaskazini “A” Mkosa wa kaskazini Unguja, juni 04,2023
Msimamizi wa majengo sBaraza la mji kaskazini “A” Hassan Abdurahman Hamdu akitoa taatifa fupi kuhusiana na ujenzi wa soko la wajasiriamali mkwajuni wakati walipotembelewa na mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa, juni 04,2023
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Abdalla Hashim Kaimu akitembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa soko la wajasiriamali unaoendelea kujengwa na chuo cha mafunzo Zanzibar wakati mbio za mwenge zilipopita katika mradi huo uliopo Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini “A” Mkoa wa Kaskazini Unguja, juni 04,2023.
Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “A” Sadifa Juma Khamis akititeta jambo na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2023 Abdalla Hashim Kaimu wakati wakitembelea mradi wa soko la mkwajuni ikiwa ni miongoni mwa harakati za mbio za mwenge,juni 04,2023.
Kiongozi wa mbio za mwenge na ujumbe wake wakikata majani wakati waliposhiriki zoezi la usafi wa Mazingira katika hospitali ya Kivunge kaskazini unguja ikiwa ni muendelezo wa mbio za mwenge mkoani humo ,juni 04,2023.
………
Na Rahma Khamis,Maelezo
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Abdalla Shaibu Kaimu amemtaka Mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa Soko la Wajasiriamali Mkwajuni kuhakikisha unakamilika kwa wakati.
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Abdalla Shaibu Kaimu amemtaka Mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa Soko la Wajasiriamali Mkwajuni kuhakikisha unakamilika kwa wakati.
Ameyasema hayo wakati alipokua akitembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa soko hilo huko Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini A mkoa wa kaskazini Unguja.
Amesema kuwa ujenzi mzuri ni ule wenye kuzingatia ubora na viwango vya hali ya juu ili wananchi wapate miradi mizuri na yenye kudumu kwa muda mrefu.
Amefahamisha kuwa lengo la matembezi hayo ni kuangalia ubora pamoja na kutambua thamanu ya fedha zilizotumika katika ujenzi huo kama zinaendana na mradi husika.
Shaibu amefafanua kuwa dhamira ya Serikali ni njema kwani inapambana kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ikiwemo za masoko ambayo yataasaidia vijana kujiwezesha kiuchumi.
Akitoa taarifa ya ujenzi wa soko hilo Msimamizi wa soko hilo Hassan Abdulrahmani Hamdu amesema kuwa soko hilo ni la Wajasirsiamali wa Mkwajuni na linatarajiwa kukamilika Agosti 2023 mwaka Msimamizi ameeleza kwamba katika soko hilo litajumuisha sehemu mbalimbali ikiiwemo milango ya maduka ,mikahawa, Ofisi ,Ukumbi wa mikutano na kibanda cha mlinzi na kuweza kuhudumia wananchi 400 hadi 500 katika Wilaya hiyo.
Ameongeza kuwa wameamua kujenga soko hilo baada ya kuona wanapata usumbufu wa kukosa mahitaji muhimu ikiwemo bidhaa za sokoni.
Ujenzi huo umegharimu zaidi ya sh za kitanzania milioni 7 na umejengwa chini ya usimamizi wa Mkandarasi kutoka Chuo cha Mafunzo ambapo ujenzi unaendelea.