Wananchi wa kijiji cha kibeni wakipanda miti ya aina mbalimbali kwaajili ya kutunza mazingira na vianzio vya maji juni 04,2023.
Wananchi mbali mbali wa Kaskazini Unguja wakifanya usafi wa mazingira katika hospitali ya kivunge mkoa wa kaskazini Unguja kuelekea maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo mei 5. hafla iliyofanyika juni 04,2023
……..
Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar.
Wananchi wa Wilaya ya Kaskazini A wametakiwa kutunza mazingira ili kuhifadhi uoto wa asili nchini.
Akifunga mafunzo ya Mabadiliko ya tabianchi Skuli ya Mkwajuni Kiongozi wa mbio za mwenge Abdala Shaibu Kaimu amesema utunzaji wa mazingira ni kitu muhimu katika nchi kwani bila mazingira hakuna maendeleo.
Amesema hivi sasa mazingira ni mabaya kutokana na wananchi kufanya uharibifu na kuchafua mazingira kutokana na shughuli mbalimbali za kijamii.
Amefahamisha kuwa mabadiliko ya tabianchi yanarejesha nyuma harakati za kimaendeleo kutokana na shughuli za kibinaadamu ikiwemo ufugaji na kilimo usiozingatia utunzaji wa mazingira, ukataji wa miti na kutupa taka ovyo.
Amefafanua kuwa mafunzo yalitolewa yatasaidia wananchi katika kutambua juu ya uhifadhi wa mazingira na kuepuka uchafuzi unaopelekea kuharibu mazingira yaliyopo.
Aidha amewapongeza vijana kwa kukubali kupatiwa elimu na kuwataka kuyafanyia kazi mafunzo hayo.
Akitoa taarifa ya mafunzo Mkufunzi wa mafunzo hayo ambaye pia ni Afisa Mazingira Wilayani humo Haji Ussi Haji amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kujifunza maana na athari za mabadiliko hayo ili wananchi wafahamu athari hizo.
Wakati huo huo Kiongozi mbio za Mwenge ametembelea Shehia ya Kibeni na kuangalia mradi wa upandaji wa miti na kusifu juhudi za wananchi katika kupambana na uhifadhi wa mazingira .
Amesema yeye binafsi ameridhia mradi huo kwani utawawezesha wananchi wa hapo kujiendesha kiuchumi.
Akitoa taarifa mradi huo mmoja wa wanakikundi cha upandaji wa miti amesema kuwa jumla ya miti 4953 imeatikwa kwa lengo la kuhifadhi mazingira na vyanzo vya maji visipotee.
Hata hivyo wanakikundi cha mradi huo wameshukuru ujio wa Mwenge wa Uhuru kwa kuridhia mradi wao na kuiomba Serikali kuendelea kukiimarisha kikundi hicho ili kurejesha uoto wa asili nchini
Jumla ya miradi minane imekaguliwa na mwenge wa uhuru katika Mkoa wa Kaskazini Unguja ambapo sehemu mbalimbali zimepitiwa na mbio hizo ikiwemo Hospitali ya Kivunge , kituo cha Afya Kidagoni na Mradi wa Visima vya maji pale