Wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Tanzania ATCL wakiwa tayari kabisa kupokea ndege katika hafla ya mapokezi ya ndege mpya ya mizigo aina ya Boeing 767 yenye uwezo wa kubeba Tani 54 kwa safari moja inayofanyika katika viwanja vya ndege vya Kimataifa vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (JNIA) leo tarehe 3/6/2023 jijini Dar es Salaam itakayopokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Hassan Suruhu (Picha na John Bukuku)
……………………….
Wafanyakazi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), viongozi wa serikali na dini pamoja na wananchi wamejipanga kupokea ndege mpya ya mizigo aina Boeing 767 inatayotarajia kutua nchini saa chache ikitokea nchini Marekani.
Wakiwa katika Viwanja vya ndege wa Kimataifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es Salaam wameonekana kuwa na furaha kubwa kutokana wanakwenda kuandika historia ya kupokea ndege hiyo yenye uwezo wa kukaa angani saa 10.
Ndege hiyo ya mizigo aina ya Boeing 767 ina uwezo wa kubebe mizigo hadi tani 54 kwa safari moja na inakwenda kuondoa adha ya wafanyabiashara waliokuwa wakipeleka mizigo yao nje ya nchi kwa ajili ya kusafirisha.
Ndege ya mizigo inatarajia kuwasili nchini leo ikiwa na marubani watatu wawili kutoka Kampuni ya Boeing iliyopo Marekani, rubani mwengine mtanzania Neema Swai wa Shirika la Ndege la ATCL .