Mratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Mkoa wa Pwani, Bi. Rose Kimaro katikati akiongozana na baadhi ya watendaji waliotembelea miradi hiyo
Moja ya miradi iliyotekelezwa na TASAF mkoani Pwani katika kata ya Utete wilayani Rufiji ni hili soko ambalo tayari linatumiwa na wananchi.
Watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar SMZ na watendajiwa wa TASAF kutoka visiwani humo wakati alipotembelea miradi TASAF inayotekelezwa Katika wilayani Rufiji.
……………………………………..
NA JOHN BUKUKU, PWANI
Mratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Mkoa wa Pwani, Bi. Rose Kimaro imeishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufanikisha kutekeleza wa miradi ambayo imekuwa msaada katika kutatua kero za wananchi.
Akizungumza Mkoani Pwani na wageni kutoka Zanzibar ambao wamekuja kujifunza mambo mbalimbali ya utekelezaji wa miradi, Bi. Kimaro, amesema kuwa kupitia TASAF Makao Makuu wamefanikiwa kutekeleza miradi mingi ambayo imeleta tija kwa Taifa.
Amesema kuwa kupitia utaratibu wa TASAF wametekeleza miradi saba ya miundombinu katika nyanja mbalimbali ambayo imewasaidia wananchi.
“Miradi hiyo ipo katika halmashauri nne kati tisa katika Mkoa wa Pwani ambayo inaendelea kutekelezwa” amesema Bi. Kimaro.
Amesema kuwa kuna miradi minne ambayo ipo katika halmashauri ya Wilaya ya Chalize ambapo kuna mradi wa jengo la kuifadhi maiti, Kibaha kuna mradi wa Zahanati na Nyumba ya Wauguzi, huku Wilaya ya Kibiti wakinufaika mradi wa Kituo cha Afya ambapo kuna majengo matano kwa sasa ambayo yapo katika hatua ya mwisho ya kukamilika.
“Tunamshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suruhu Hassani kwani katika Mkoa wa Pwani miradi hii imetusaidia sana kwani wananchi walikuwa wanapata shida kutokana na changamoto na ukosefu wa miundombinu” amesema Bi. Kimaro.
Amesema kuwa katika kipindi kifupi Mkoa wa Pwani wamepiga hatua kubwa kiuchumi kutokana miradi ambayo imekuwa msaada mkubwa katika kufanikisha shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
“Nawashukuru wageni kutoka Zanzibar kwa kuja kujifunza mambo mengi katika Mkoa wa Pwani” amesema Bi. Kimaro.