Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba (wa
kwanza,kushoto), na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Fedha la Kimataifa
(IMF) nchini Tanzania, Jens Reinke (wa Pili kutoka kulia) wakiwa
katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma tarehe 2 Juni, 2023. Wengine
ni watendaji kutoka Wizara ya Nishati, TPDC na IMF
Kamishna wa Petroli na Gesi, Michael Mjinja (wa kwanza kushoto)
pamoja na watendaji kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania
(TPDC) wakiwa katika kikao cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati,
Mhandisi Felchesmi Mramba (hayupo pichani) na Mwakilishi Mkazi wa
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) nchini Tanzania, Jens Reinke
(hayupo pichani kulia).
Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga akiwakatika kikao cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati,Mhandisi Felchesmi Mramba (hayupo pichani) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) nchini Tanzania, Jens Reinke (hayupo pichani)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba (wa tatu
kushoto) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF)
nchini Tanzania, Jens Reinke (wa nne kutoka kulia) wakiwa katika
picha ya pamoja na watendaji wa Wizara ya Nishati, Shirika la
Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na IMF baada ya kikao
kilichofanyika jijini Dodoma tarehe 2 Juni, 2023.
………………………..
Teresia Mhagama na Godfrey Mwemezi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) nchini Tanzania, Jens Reinke na watendaji wengine wa
Shirika hilo ambapo kikao hicho kililenga kujadili masuala mbalimbali ikiwemo mwenendo wa uchumi, utekelezaji wa bajeti, mipango ya maendeleo ya nchi na program ya ufadhili wa miradi (ECF).
Kikao hicho kimefanyika jijini Dodoma tarehe 2 Juni, 2023 na
kuhudhuriwa na Kamishna wa umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi
Innocent Luoga, Kamishna wa Petroli na Gesi, Michael Mjinja,
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania
(TPDC), Mussa Makame na watendaji wengine kutoka Wizara ya Nishati na
TPDC.
Katika kikao hicho, Mhandisi Mramba aliwaeleza watendaji hao kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali itakayopelekea nchi kuwa na umeme wa kutosha na uhakika ukiwemo mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) utakaozalisha megawati 2,115, unaotarajiwa kukamilika mwezi Juni 2024.
Katibu Mkuu pia amewaeleza watendaji hao kuhusu Mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia (LNG) ambao ameeleza kuwa, majadiliano yake ya
Mkataba wa Nchi Hodhi (HGA) na Mkataba wa Uzalishaji na Ugawanywaji Mapato (PSA) kati ya Timu ya Majadiliano ya Serikali na Wawekezaji katika Vitalu husika yamekamilika.
Vilevile, amewaeleza watendaji wa IMF kuhusu hatua zinazoendelea
kufanyika katika mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki
(EACOP) ambao alisema kuwa kwa ujumla unaendelea vizuri.
Aidha, amewaeleza watendaji hao kuhusu hatua mbalimbali ambazo
Serikali imezifanya hadi sasa za kuimarisha matumizi ya nishati safi
ya kupikia ili ifikapo mwaka 2033, asilimia 80 ya wanachi wawe
wanatumia nishati hiyo.
Katibu Mkuu pia ametanabaisha kuhusu vyanzo vya nishati jadidifu
vilivyopo nchini ikiwemo Jua na Upepo ambavyo amesema kuwa, wawekezaji mbalimbali wanaweza kuvitumia kuzalisha umeme.
Katibu Mkuu ameishukuru IMF kwa kutoa fedha shilingi Bilioni 200
kupitia mpango wa ECF kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kuimarisha
gridi ya Taifa pamoja na kupeleka umeme katika vitongoji vya mikoa ya
Songwe na Kigoma.
Kwa upande wake, Mwakilishi Mkazi wa IMF nchini Tanzania, Jens Reinke
amemshukuru Katibu Mkuu kwa kupata taarifa hizo muhimu ambazo wao kama wadau zinawasaidia katika kufahamu mwelekeo wa Serikali katika utekelezaji wa miradi mbalimbali