Serikali ya awamu ya Sita imeendelea kuunga mkono juhudu za wanafunzi wanaofanya vizuri masomo ya Sayansi kidato cha 4 na 6 katika mitihani yao ya kitaifa ambapo leo Ofisi ya Mkemia mkuu wa serikali imetoa ya vyeti na Zawadi kwa wanafunzi waliofaulu nafasi ya Kwanza hadi ya tatu kitaifa katika Masomo ya Sayansi (Baiolojia, Fizikia na Kemia) leo tarehe 1 June katika sherehe zilizofanyika katika kituo cha kimataifa cha mikutano cha Julius Nyerere.
Jumla ya wanafunzi thelathini na sita(36)ambao Kumi na nane(18) kidato cha nne(4) na kumi na nane(18) kidato cha sita 2021 na 2022 pamoja na waalimu sita(6)
wamekabidithiwa vyeti pamoja na zawadi .
Akiongea baada ya kukabidhi vyeti hivyo Mganga mkuu wa Serikali ambaye alikuwa mgeni Rasmi Profesa Tumaini Nagu amewapongeza wanafunzi hao kwa jitihada kubwa walizozionyesha na kuwahaidi Serikali ya awamu ya 6 itawapa ushirikiano asilimia mia kuhakikisha wanatimiza ndogo zao huku akiipongeza ofisi ya Mkemia mkuu wa serikali kuandaa sherehe za kuwapongeza wanafunzi hao ambazo zilianzishwa tangia mwaka 2007 na zimeweza kuwapa hamasa wanafunzi kuendelea kufanya vizuri katika masomo ya sayansi.
Ameongeza kwamba serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kutambua umuhimu wa taaluma ya Sayansi inaendelea kuboresha mazingira rafiki ya kusoma kwa vitendo katika shule na vyuo mbali hapa nchini
Ameongeza kwamba Serikali kupitia Wizara ya Afya inatambua kazi kubwa inayofanywa na ofisi ya Mkemia mkuu wa serikali kwa kutambua na kuona umuhimu wa kuandaa sherehe za pongezi kwa wanafunzi wanaofanya vizuri vizuri, hata prof Nagu ametoa maoni kwa Mamlaka hiyo kuangalia namna ya kuongeza Somo la hisabati katika sherehe za miaka ijayo kwani kwenye maisha hisabati pia inachukua nafasi kubwa.
Aidha Profesa Nagu ametumia nafasi hiyo pia kuwahasa wanafunzi hao kwenda kuwa mfano wa kuigwa kwa jamii, kuwa na maadili mema na kuendelea na juhudi katika kuhakikisha wanatimiza Malengo yao lakini pia kuepuka vishawishi mbali mbali ikiwemo kuchukua tahadhari juu ya maambukizi ya virusi vya ukimwi na magonjwa ya zinaa kwa ujumla.
Kwa Upande wake Mkemia mkuu wa serikali Dkt Fidelice Mafumiko amewapongeza wanafunzi hao kwa ufaulu mzuri lakini amewapongeza waalimu wazazi na walezi kwa kuhakikisha wamewapa wanafunzi hao ushirikiano tangia walipoanza masomo hadi walipomaliza na kuonyesha matokeo mazuri huku akihaidi ofisi hiyo itaendelea kutoa zawadi zawadi mbali mbali kwa watainiwa watakaofanya vizuri katika masomo ya Sayansi hata hivyo ameongeza kwamba Mamlaka hiyo kwa kutambua Umuhimu wa Masomo ya Sayansi inatoa ushirikiano kwa kuwapatia Wanafunzi nafasi za kujifunza kwa vitendo katika vyuo.
Naye Mwalimu Richard Masanja amesema anaishukuru Ofisi ya Mkemia mkuu wa serikali kwa kutambua mchango wao na kuwapatia vyeti na kuwaandaa sherehe kwao ni chachu na wanahaidi kufundisha kwa bidii zaidi kuhakikisha wanafunzi wengi wanapata ufaulu mzuri katika masomo hayo ya Sayansi.
Hata hivyo mwalimu Richard ameiomba Mamlaka hiyo kuangalia namna ya kuanzia kuchambua wanafunzi waliofaulu masomo hayo kuanzia Ngazi ya mkoa kwani kufanya hivyo itaongeza hamasa zaidi kwa wanafunzi wengi.