Afisa Mtendaji Mkuu Ofisi ya Mipaka ya Kimataifa Kenya (KIBO) Juster Mkoroi (wa pili kushoto) akisisitiza jambo wakati timu ya wataalamu wa Tanzania na Kenya ilipotembelea eneo la mpaka katika mto Losoyai wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro tarehe 30 Mei 2023. Wa tatu kushoto ni Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Hamdouny Mansoor na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mwanga Abdalah Mwaipaya.
Mratibu wa zoezi la uimarishaji mpaka wa kimataifa kati ya Tanzania na Kenya Joseph Ikorongo pamoja na wataalamu wa nchi hizo mbili wakiangalia muelekeo wa mfereji wa maji yanayotoka mto Losoyai wakati wataalamu wa nchi hizo walipotembelea eneo hilo tarehe 30 Mei 2023.
Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Hamdouny Mansoor (Kushoto) akitoa maelezo kwa timu ya wataalamu wa Tanzania na Kenya walipotembelea eneo la mto Losoyai wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro tarehe 30 Mei 2023.Timu ya wataalamu kutoka Kenya na Tanzania ikielekea eneo la mto Losoyao kuangalia alama ya mpaka wa kimataifa baina ya nchi hizo tarehe 30 Mei 2023.
Ujumbe wa Kenya ukiwa katika kikao cha pamoja kati ya Tanzania na Kenya kujadili uimarishaji mpaka wa nchi hizo tarehe 31 Mei 2023.
Ujumbe wa Tanzania ukiwa katika kikao cha Kamati ya pamoja kati ya Tanzania na Kenya kujadili uimarishaji mpaka wan chi hizo tarehe 31 Mei 2023.Ka
Kimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha David Lyamongi akizungumza wakati wa kufungua Kikao cha Kamati ya Pamoja cha Uimarishaji Mpaka wa Kimataifa kati ya Kenya na Tanzania jijini Arusha tarehe 31 Mei 2023.
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha David Lyamongi (Katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Tanzania na Kenya unaoshiriki kikao cha Kamati ya Pamoja baina ya nchi hizo jijini Arusha tarehe 31 Mei 2023.
……………………
mto Losoyai unaoungana na Ruvu kuingia ziwa Jipe na kufuatiwa na mpaka wa nchi kavu hadi Pangani wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro kwa lengo la kujiridhisha.
Wakiwa katika eneo hilo, timu hiyo ya wataalamu ya Kamati ya Pamoja ya nchi hizo wakioongozwa na Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Hamdouny Mansoor kwa upande wa Tanzania na Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Mipaka ya Kimataifa ya Kenya (KIBO) Juster Nkoroi walijionea uhalisia wa mpaka pamoja na changamoto za eneo hilo wakati wa ukaguzi.