Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria katika kikao na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi, Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye.
Kikao hicho kilichofanyika leo tarehe 01 Juni, 2023 katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma kilikuwa kwa ajili ya kujadili Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali yatokanayo na Urekebu wa Sheria wa Mwaka 2023 (The Laws Revision (Miscellaneous Ammendments) Bill, 2023).