Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umetoa wito kwa wastaafu, wanachama wa Mfuko huo na wananchi kwa ujumla kufika kwenye banda lao katika Maonesho ya Biashara na Utalii katika viwanja vya Mwahako jijini Tanga ili kuhudumiwa na kupata Elimu ya Hifadhi ya Jamii.
Maonesho hayo ambayo yamefunguliwa rasmi leo Mei 31, 2023, na Bw. Conrad John Milinga, Kaimu Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara timu ya PSSSF, ikiongozwa na Meneja wa Kanda ya Kaskazini Bi Vones Koka, iko tayari kuwahudumia wanachama na wananchi kwa ujumla.
Akizungumzia Huduma zitolewazo na PSSSF katika band Hilo, Bi. Vones . Kola alisema mwanachama atafurahia huduma kama ambazo amekuwa akipata kwenye Ofisi za Mfuko zilizoenea kote nchini.
Alizitaja kuwa ni pamoja na Mwanachama kupata taarifa za michango yake, Mstaafu kuhakiki taarifa zake, Elimu ya mafao yanayotolewa na Mfuko na fursa za uwekezaji.” Alifafanua.
Akieleza zaidi, alisema muitikio wa watu kutembela banda hilo ni mkubwa
“Kwa kweli wengi walijitokeza katika maonesho hayo, na wengi waliofika katika banda letu walikuwa wakifuatilia taarifa za michango yao na pensheni” alisema Bi. Vones Koka
Kwa upande wake Mkuu wa ofisi ya Tanga, Bw. Selemani Majingo alisema Mkoa wa Tanga ni miongoni mwa mikoa yenye idadi kubwa ya wanachama wa PSSSF.
“Kurahisisha utoaji huduma tuna ofisi ndogo katika wilaya ya Korogwe, lengo likiwa kuwasogezea huduma wanachama wetu, pamoja na wingi wa wanachama tumejipanga vyema na tunatoa huduma sahihi kwa wote”. Alisema.
PSSSF hushiriki katika maonesho mbalimbali kwa lengo la kuwafikia wanachama na wananchi kwa lengo la kutoa elimu na huduma.
Maonesho
hayo yaliyobeba kauli mbiu isemayo “Kilimo, Viwanda, Utalii na Madini ndio
msingi wa maendeleo ya kiuchumi” yameanza Mei 28 na yatafikia kilele Juni 6,
2023