Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Profesa Makame Mbarawa
Na Ahmed Mahmoud.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Profesa Makame Mbarawa amewaagiza wataalam wabobezi wa barabara kutoka ndani na nje ya nchi kufanya uchambuzi na kuishauri serikali juu ya matumizi sahihi ya matairi mapana kwa matumizi ya barabara za Tanzania.
Profesa Mbarawa alitoa agizo hilo jana Jijini Arusha wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Usafiri Endelevu wa Mizigo ya Barabara kwa Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii iliyoshirikisha wataalam wabobezi kutoka ndani na nje ya nchi.
Alisema endapo wataalam hao wakitoa tathimini ya matumizi ya barabara hizo kwa kuanisha faida na hasara zake kwani serikali inataka kuandaa sera ya matumizi ya tairi hizo lakini lazima ipate data (taarifa za kitaalam)ili wajue faida na hasara zake .
Alisema pia wataalam hao watajadili usafirishaji wa mizigo inayotumiw barabara na kuleta msongamano wa magari ingawa serikali inajenga reli ya kisasa ya SGR kwaajili ya kupunguza msongamano wa malori barabarani kwakutumia reli.
” tunataka kujua tukitumua matairi mapana lakini lazima tujue faida na hasara zake ili tufanye maamuzi sahihi kwaajili ya matumizi sahihi ya barabara “