Sehemu ya Umati wa Wafanyabiashara wa Soko la Nyanya Ilula na Wakazi wa eneo hilo wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo.
Katibu Mkuu ameambatana na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema na Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Haji Ussi Gavu kwenye ziara ya kikazi mkoani Iringa.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema akizungumza na wakina mama juu ya uboreshwaji wa huduma za afya ya mama na mtoto alipotembelea kituo cha afya Ilula jimbo la Kilolo mkoani Iringa ikiwa sehemu ya ziara ya kikazi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo.