Mkuu wa wilaya ya Same Bi.Kasilda Mgeni ametoa pongezi na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia wilaya ya Same Fedha nyingi lengo likiwa kuhakikisha Miradi yote ya Same inakamilika kwa wakati na kuanza kutumiwa na wananchi.
DC Kasilda amesema kuwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan amewafuta machozi Wananchi wa Same kwa kilio kikubwa cha Maji hivyo amehakikisha Wananchi wa wilaya ya Same wanapata maji kwa Kutokana na MIRADI ya maji inayotekelezwa na Ruwasa wilaya ya Same huku Mradi mkubwa wa Maji Mwanga Same Korogwe ukiwa imekamilika ukihueumia wakazi WA wilaya ya Same mpaka kufikia asilimia 90
Aidha amewaomba wananchi wote wa wilaya Same kuendelea kuunga mkono juhudi za Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa Kazi kubwa anayoifanya Hapa Nchini na kuhakikisha Miradi yote ya Same vituo vya Afya barabara za zinazohudumiwa na Tarura ambapo pia baadhi ya shule zinakamilika kwa wakati na kuendelea kupokea wanafunzi ili kuendeleza na masomo.