Afisa Mkuu wa Kampuni ya Tigo Kitengo cha TIGOPESA Angelica
Pesha (wapilikulia), akishikana mikono na Meneja wa kampuni ya Uber ukanda wa afrika
mashariki Imran Mnji wakati wa hafla ya kutangaza ubia wakufanya kazi pamoja kwa muda wa mwaka mmoja wa kampeni ya kutoa zawadi kwa madereva na wasafiri watakao tumia Uber na Tigopesa wengine kushoto ni Meneja Uendeshaji wa Uber Monica Mziray pamoja na Afisa kutoka kampuni ya tigo. Hafla Hiyo imefanyika leo jijini
Dar es Salaam.Afisa Mkuu wa Kampuni ya Tigo Kitengo cha TIGOPESA Angelica
Pesha akizungumza wakati wa hafla ya ya kutangaza ubia wakufanya kazi pamoja na kampuni ya Uber Tanzania kwa muda wa mwaka mmoja wa kampeni ya kutoa zawadi kwa madereva na wasafiri watakaotumia Uber na Tigopesa .
Meneja Uendeshaji wa Uber .
…………………..
Monica Mziray akizungumza wakati wa hafla ya kutangaza ubia wakufanya kazi pamoja na kampuni ya tigo kwa muda wa mwaka mmoja wa kampeni ya kutoa zawadi kwa madereva na wasafiri watakaotumia Uber na Tigopesa .
Kuanzia sasa, madereva wanaotumia mfumo wa Uber wanaweza
kujisajili kama wakala wa Lipa kwa Simu ya Tigo Pesa, ambayo itawawezesha kupokea nauli kutoka kwa wasafiri watakaopenda kulipa nauli zao kupitia mitandao ya simu.
Madereva wanaotumia
mfumo wa Uber wataweza kupata pesa zao kutoka kwenye akaunti za Lipa kwa Simu bila makato yoyote kutoka kwenye mawakala wa Tigo Pesa kwa kiasi chochote chini
ya Tshs. 500,000 kwa siku.Abiria watakaotumia huduma ya Lipa kwa Simu ya Tigo pesa watarudishiwa 10% ya nauili watakayolipa kwenye akaunti zao za Tigo Pesa, sambamba na kampeni hii, Uber itaendelea kufanya kampeni zingine kupitia app
yao.
Madereva watakaotumia
huduma ya Lipa kwa Simu kwa malipo yao ya nauli watarudishiwa 20% ya ada ya malipo kwa kila muamala unaofanywa kupitia Lipa Kwa Simu.Meneja wa Uber Afrika
Mashariki, Bw Amran Manji anasema, “Tuna furaha kubwa kuingia Ubia na kampuni ya Tigo katika kufanikisha kampeni hii itakayowasaidia madereva kuongeza kipato, na pia abiria kuokoa pesa kila wanapotumia mfumo wa Uber.
Ubia huu ni muhimu na una tija kubwa kwa sababu inawafanyia
wepesi abiria na madereva kufanya miamala wanapotumia mtandao Uber, ikiwa ni pamoja na wateja ambao hawana akaunti za benki na wamepungukiwa na pesa taslimu.”Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Pesa, Bi. Angelica Pesha amesema: “Ubia huu tunaoingia na kampuni ya Uber unaonesha waziwazi nia ya Tigo Pesa
kufanikisha malengo yake ya kusambaza huduma za kifedha katika jamii ya Watanzania.
Sasa madereva wa Uber
watapata huduma watapata huduma ya malipo ambayo inahakikishia abiria wao njia salama na rahisi ya kulipa nauli wanaposafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Sambamba na hilii, ubia huu ni ushahidi kwamba huduma ya Lipa Kwa Simu ni huduma yenye ufanisi mkubwa na tunategemea kwamba huduma hii itasaidia biashara ndogondogo kuendele kukua.
”Sekta ya usafiri wa teksi za
mitandaoni imeleta mageuzi makubwa katika namna ambayo tunasafiri katika miji yetu, na tangu walipofungua milango yao jijini Dar es Salaam mwaka 2016, Uber amekuwa mshirika mkubwa wa jiji hilli kupitia huduma za usafiri, kuchangia katika uchumi kwa kutoa fura za kiuchumi sambamba na kuchangia katika mapato ya
serikali.
Amran anahitimisha kwa kusema,
“Tuna matumaini makubwa na soko ka Tanzania na kunzishwa kwa programu kama hizi zitachochea ukuaji wa biashara, sambamba na kuimarisha ubora wa huduma kwa
abiria.”
Kuhusu Uber Dhamira ya Uber ni
kuwasaidia watu kutumia simu ili kupata usafiri – kila mtu na mahali popote.
Tulianza mwaka 2009 kwa kutafuta ufumbuzi wa tatizo dogo: unawezaje kutumia simu yako kuita usafiri? Baada ya kufanya zaidi ya safari bilioni 10, tumeanza kutafuta ufumbuzi wa tatizo kubwa zaidi: kupunguza foleni ya magari na uchafuzi wa mazingira katika miji mbalimbali kwa kutumia magari machache kusafirisha watu wengi Uber inatoa huduma zake katika miji zaidi ya 60 Kusini mwa Jangwa la Sahara
(Cape Town, Durban, Joburg, Pretoria, Gqeberha (zamani ikijulikana kama Port Elizabeth), East London, Polokwane, Cape West Coast, Worcester, Emalahleni / Middelburg, Garden Route, Rustenburg,
Potchefstroom, Mbombela (zamani ikijulikana kama Nelspruit), Newcastle, Mthatha, Thohoyandou, Upington, Margate, Richards Bay, Welkom, Phuthaditjhaba, Ermelo, Queenstown, Nairobi, Mombasa, Nakuru, Ibadan, Warri, Owerri and Akure Enugu, Kano, Port Harcourt, Lagos, Abuja, Benin City, Abidjan, Kampala, Accra, Kumasi, Tamale na Sunyani). Kwa ujumla, huduma za Uber zinapatikana katika
miji zaidi ya 10 000 katika nchi 65. Ili msafiri aweze kuita gari To request a
ride, users must download the free application for Android, iPhone, Blackberry 7, or register for Uber at www.uber.com/go.
Uber
inatoa huduma zake katika miji kumi na tatu Kusini mwa Jangwa la Sahara (Cape Town, Durban, Joburg, Pretoria, Port Elizabeth, Nairobi, Mombasa, Lagos, Abuja,
Kampala, Accra, Kumasi and Dar es Salaam). Kwa jumla mtandao wa Uber
unapatikana katika miji zaidi ya 600 na zaidi ya nchi 65. Ili msafiri aweze
kuita gari, ni lazima aweke app ya Uber ya simu za Android, iPhone, Blackberry
7, au ajiandikishe kutumia Uber kupitiawww.uber.com/go. Kwa maswali tafadhali tembeleawww.uber.com