Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe (kulia) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) DKt. Tedros Adhanom Ghebreyesus (kushoto) mara baada ya kushiriki kwenye kikao cha pamoja kati ya ujumbe kutoka Tanzania na WHO. Ujumbe kutoka Tanzania wakiongozwa na Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Marzui wapo Jijini Geneva Uswisi kwenye kikao cha 76 cha Shirika la Afya Duniani.
Wiaziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Marzui (kulia) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) DKt. Tedros Adhanom Ghebreyesus (kushoto) mara baada ya kushiriki kwenye kikao cha pamoja kati ya ujumbe kutoka Tanzania na WHO. Ujumbe kutoka Tanzania wakiongozwa na Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Marzui wapo Jijini Geneva Uswisi kwenye kikao cha 76 cha Shirika la Afya Duniani.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu (kulia) kwenye picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) DKt. Tedros Adhanom Ghebreyesus (kushoto) mara baada ya kushiriki kwenye kikao cha pamoja kati ya ujumbe kutoka Tanzania na WHO. Ujumbe kutoka Tanzania wakiongozwa na Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Marzui wapo Jijini Geneva Uswisi kwenye kikao cha 76 cha Shirika la Afya Duniani.
Picha ya pamoja ya viongozi na watendaji wa Sekta ya Afya nchini wakiwemo Mhe. Nassor Marzui Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe. Stanslaus Nyongo Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya Ukimwi, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe, Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu pamoja na watendaji kutoka Shirika la Afya Duniani wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Tedros Adhanom.
………………………….
Katibu Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus ameipongeza Tanzania kwa juhudi inazoendelea kufizanya katika kupambana na kudhibiti magonjwa ya mlipuko kuingia na kuenea nchini Tanzania.
Dkt. Tendros amesema hayo kwenye kikao maalum na ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Marzui pamoja na viongozi wengine waandamizi wakiwemo Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe, Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu pamoja na wataalam wengine katika Sekta ya Afya.
Dkt. Tedros ameipongeza Tanzania kwa mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Marburg na kwa kushirikiana na WHO katika kuimarisha huduma za uchunguzi na udhibiti dhidi ya magonjwa ya mlipuko.
“Tunaendelea kuipongeza Tanzania kwa juhudi zinazoendelea kufanywa na Serikali kwa ushirikiano na WHO katika kuwaendeleza kitaaluma wahudumu wa Afya ngazi ya jamii na kukubaliana kwa pamoja kuboresha huduma za afya ngazi ya msingi ili kuweza kudhibiti magonjwa ya mlipuko katika hatua za awali na kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza” amesema Dkt. Tendros.
Tanzania imeungana na nchi nyinginezo wanachama wa Umoja wa Mataifa chini ya Shirika la Afya Duniani kushiriki kikao hiki muhimu cha 76 cha Shirika la Afya Duniani kinachofanyika Geneva, Uswisi.