Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeshiriki katika Tamasha la kudumisha na kuhifadhi Mila na Tamaduni za Kiafrica kwa ajili ya kizazi kijacho ambapo Bi Esta Solomoni ,
Mkuu wa ofisi ya TTB kanda ya Kaskazini alipata nafasi ya kutoa wasilisho kuhusu utamaduni za kitanzania, vivutio vya utalii vya Tanzania pamoja na fursa za Uwekezaji zilizopo katika sekta ya utalii.
Tamasha hili la siku tano (5) limefanyika katika Makumbusho ya Viumbe jijini Arusha kuanzia tarehe 22 – 27 Juni, 2023. Tamasha limeweza kuvutia washiriki kutoka nchi za Afrika Kusini, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Zimbabwe, America,
Ujerumani, Uingereza ,Costa Rica, Morocco, Nigeria, Ghana, Senegal, Taiwan, Zanzibar, Congo DRC, Ufaransa, Uholanzi, Burkina Faso, Cote D’Ivoire, Benin na Jamaica.
Aidha, Washiriki wameweza kushiriki zoezi la kupanda miti na kupata burudani za muziki na ngoma za utamaduni wa Makabila ya Tanzania. Bodi ya Utalii Tanzania inaendelea na mkakati wake wa kutangaza utalii kupitia matukio ya Kitaifa na kimataifa yanayofanyika nchini Tanzania.