Ubalozi wa Tanzania Afrika Kusini umejumuika na balozi nyingine za Afrika zinazowakilisha nchi zao nchini Afrika Kusini katika kuadhimisha miaka 60 ya Umoja wa Nchi Huru za Afrika OAU na taasisi iliyoundwa baada yake, Umoja wa Afrika “Siku ya Afrika Duniani”.
Katika maadhimisho hayo, Ubalozi wa Tanzania chini ya uongozi wa Mhe.Maj.Jen.(Mst) Gaudence S.Milanzi,Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini ulishirikiana na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo katika Ujumbe ulioongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Saidi Yakubu, na Bi Fatma Hamad Rajab,Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Kikundi cha Sanaa cha Safi kutoka Tanzania kilitumbuiza na kutia fora katika maadhimisho hayo.