K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MWANZA
MADAKTA
wameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wake Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweka mazingira
rafiki na mazuri kuhakikisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) unatekeleza
malengo yake ya ulipaji wa fidia kwa wafanyakazi wanaoumia, kuugua ama kufariki
kutokana na kazi.
Wameyasema
hayo jijini Mwanza mwishoni mwa kikao kazi kilichoandaliwa na WCF kuwajengea
uelewa madaktari kutoka mikoa ya Kanda ya ziwa kuhusu namna ya kufanya tathmini
ya ulemavu na magonjwa yatokanayo na kazi.
“Napenda
kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweka mazingira
rafiki na mazuri kuhakikisha WCF inaweza kutekeleza malengo yake kwa maana ya
kuhudumia watumishi wa sekta ya umma na sekta binafsi wanaoumia au kuugua
kutokana na kazi.” Alisema Dkt. Pasclates Ijumba kutoka Hospitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Geita.
Alisema
mafunzo hayo yamewawezesha kuelewa kuwa madaktari wanahusika katika mchakato wa
kusaidia WCF kulipa fidia stahiki kwa kufanya tathmini sahihi
“Nitakachokisaidi
kwa Mfuko ni kuhakikisha nafanya tathmini ya kina kwa mgonjwa ili aweze kupata
stahiki zake lakini bila kuuonea Mfuko.” Amesema Dkt. Charles Makoye kutoka
Hospitali ya Wilaya Maswa.
Naye
Dkt. Noel Saitoti kutoka Hospitali ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera alisema
licha ya ukweli kwamba WCF ina muda mfupi wa miaka minane tangu kuanzishwa
kwake lakini imeshakuwa role model (mfano wa kuigwa) kutokana na mifumo yake
mizuri ya utoaji huduma na kuzipita nchi nyingi za Afrika zilizotangulia muda
mrefu kwenye sekta ya utoaji fidia kwa wafanyakazi.
Alisema
mafanikio hayo kwa kiasi kikubwa yametokana na serikali ya awamu ya sita chini
ya uongozi wake Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ambaye kupitia Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
inayosimamia Mfuko huu, imeuwezesha Mfuko kutekeleza vema majukumu yake.
“Nimesoma
kwenye vyombo vya habari kwamba Afrika Kusini, Kenya na Zambia zimekuja
Tanzania kujifunza kutoka WCF, hii ni heshima kubwa kwaMfuko lakini kwa nchini
yetu.” Alisema Dkt. Saitoti.
Aidha
madaktari hao pia wameipongeza WCF kwa namna inavyotumia teknolojia (TEHAMA)
kurahisisha utoaji wa huduma.
“Mchakato
wa utoaji taarifa unaishia online, mwajiri hahitaji kwenda ofisi za WCF
anachotakiwa ni kuingia kwenye mfumo na kutuma taarifa ya tukio WCF na Mfuko
unapata taarifa siku hiyo hiyo ya tukio.” Amesema Dkt. Raphael Kibata kutoka
Hospitali ya Wilaya Butiama.
Akizungumza
wakati wa kuahirisha kikao kazi hicho, Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw.
Balandya Elikana, aliwaasa madaktari hao kuzingatia maadili ya kazi zao
wanapotekeleza wajibu wa kufanya
tathmini ya ulemavu (Impairment Assessment) kwa wafanyakazi walioumia au kuugua
kutokana na kazi.
“Kwa
kufanya hivyo mtausaidia mfuko kutoa fidia stahiki na kwa wakati, ninaamini
mkifika kwenye maeneo yenu mtaenda kufanya kwa vitendo” Alisema.
Alisema
Mfanyakazi akiwa na uhakika wa kinga ya kipato chake atafanyakazi kwa bidii na
kujituma kwani anajua hata akiumia kiko chombo kitakachosimamia maisha yake na
familia yake.
Akizungumza
kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu WCF, Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini WCF, Dkt.
Abdusalaam Omar alisema Mafunzo hayo yamejikita kwenye maeneo makubwa mawili
ambayo ni pamoja na kuwawezesha madaktari kuweza kubaini magonwja yatokanayo na
kazi.
“Sehemu
ya pili ni kuwawezesha madaktari kufanya tathmini ya ulemavu wa kudumu na kujua
mfanyakazi aliyeumia au aliyepata ugonjwa unaotokana na kazi ana asilimia ngapi
kutokana na madhara aliyoyapata.” Alifafanua.
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw. Balandya Elikana akizungumza na madaktari hao.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge (kulia) akimkabidhi stika, mshiriki kutoka Shinyanga, Dkt. Mariaconsolata kama ishara ya kukamilika mafunzo. Stika hizo zitatumika kubandikwa kwenye hospitali wanakotoka washiriki ili kuonyesha kuwa Wataalamu wa Tathmini wanapatikana kwenye hospitali husika.
Mgeni rasmi
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw. Balandya Elikana
akikabidhi cheti mmoja wa wahitimu wa mafunzo.