Mradi huo utaanza katikati ya jiji, kutoka kituo cha mabasi cha Mnazi Mmoja barabara ya Ali Hassan Mwinyi na Barabara ya Bagamoyo hadi Tegeta na Boko
Aidha serikali imetoa shilingi bilioni 570.6/- ($248.1m) kwa ajili ya kutekeleza BRT Awamu ya tatu na nne ambapo awamu ya III inahusisha ujenzi wa barabara ya kilomita 23.6 kutoka Gongolamboto hadi katikati ya jiji, kando ya Barabara ya Nyerere, na sehemu ya Barabara ya Uhuru kutoka Tazara hadi Kariakoo-Gerezani