Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)
kupitia kwa Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama,
Mhe Peter Kazadi ameikabidhi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tuzo ya Heshima (Gardons notre amitié) – inayohusu KUDUMISHA UHUSIANO
baina ya Nchi hizo mbili .Tuzo hiyo imepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini
DRC, Mhe. Said J Mshana wakati wa Sherehe za Miaka 60 ya Umoja wa
Afrika iliyoandaliwa kwa ajili ya Mawaziri wa SADC waliohudhuria Mkutano kuhusu
Udhibiti wa Maafa.
|
Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mhe Said J Mshana akiongea jambo baada ya kukabidhiwa Tuzo na Serikali ya DRC |
Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mhe Said J Mshana alimwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera, Bunge na Uratibu katika kikao cha Mawaziri wa SADC kilichohusu udhibiti wa maafa kilichofanyika jijini Kinshasa.
Hadi kufikia tarehe 25 Mei 2023, Nchi Wanachama sita kati ya kumi na sita zilikuwa zimesaini Mkataba wa Uendeshaji wa Kituo cha Operesheni na Huduma za Kibinadamu cha SADC. |
|
|
Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mhe Said J Mshana katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano wa Mawaziri wa SADC uliohusu udhibiti wa maafa uliofanyika jijini Kinshasa |