Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo amewasili Mafinga, wilaya ya Mufindi mkoani Iringa tayari kwa ziara ya siku 7 akiwa ameongozana na Wajumbe wawili wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Haji Ussi (Gavu) na Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjemahapaakizungumamzanawana viongozi wa CCM mkoa wa Iringa na wanachama wa CCM kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Ndugu Daud Yasin.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Isimani Ndugu William Lukuvi mara baada ya kupokelewa na viongozi mbalimbali wa CCM mkoani Humo leo.
Ndugu Sophia Mjema Katibu wa NEC itikadi na Uenezi akiunguma mara baada ya ujumbe wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo kuwasili mkoani Iringa kwa ziara ya siku 7.