Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na Mameneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha Mameneja hao na Waziri huyo jijini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa (katikati), akiteta jambo na Mkurugenzi wa Barabara kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Eng. Aloyce Matei mara baada ya kumaliza Kikao kazi kilichowakutanisha Mameneja Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), na Waziri huyo jijini Dodoma. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Rogatus Mativila.
Sehemu ya Menejimenti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha Mameneja wa TANROADS na Waziri huyo jijini Dodoma.
Mameneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha Mameneja hao na Waziri huyo jijini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa (katikati) akisalimiana na Mameneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mara baada ya kumaliza kikao kazi kilichowakutanisha Mameneja hao na Waziri huyo jijini Dodoma.