Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera akiwa katika matembezi ya hisani ya kuchangia ujenzi wa hosteli ya wanafunzi wakike wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Mbeya. Matembezi hayo yalianzia Kituo cha Basi cha Kabwe jijini mbeya hadi viwanja vya ndaki hiyo eneo la Forest leo Mei 25, 2023.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa William Mwegoha akitoa taarifa ya chuo na kuelezea umuhimu wa harambee ya ujenzi wa Hostel ya wanafunzi wakike katika Ndaki ya Mbeya leo Mei 25, 2023
Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo,(Taaluma Utafiti na Ushauri) Dkt. Eliza Mwakasangula akitoa neno la Shukrani kwa niana ya Menejimenti na Wanajumuiya katika harambee ya ujenzi wa Hostel ya wanafunzi wakike katika Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Mbeya leo Mei 25, 2023
Mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu Shahada ya Kwanza ya Menejimenti ya Rasilimali Watu, Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Mbeya, Neema Alex akielezee changamoto alizopitia alipokuwa akikaa nje ya Chuo na umuhimu wa ujenzi wa hosteli hizo katika haramee ya ujenzi wa Hosteli za wanafunzi wa kike Chuoni hapo leo Mei 25, 2023.
Washiriki wa matembezi ya hisani ya kuchangia ujenzi wa hostel ya Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Mbeya wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera.
Mwanafunzi wa darasa la Tano, Shule ya Msingi Ndola Mbalizi Abubakari Shabani Mwamba akichangia shilingi 400 katika harambee ya ujenzi wa hosteli za Kike Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Mbeya. Na kuwaomba wananchi wa Mkoa wa Mbeya na vitongoji vyake kumuunga mkono Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera kwenye harambee hiyo
……
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera amewataka wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo Taasisi za Serikali, Sekta binafsi, Wafanyabiasha pamoja na Wananchi kuchangia harambee ya ujenzi wa hosteli za wanafunzi wa kike Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ambao utagharimu Shillingi bilioni 5.8.
Akizungumza leo tarehe 25/5/2023 Mkoani Mbeya katika uzinduzi wa harambee iliyokwenda pamoja na matembezi ya hisani, Mhe. Homera amesema kuwa kila mmoja anapaswa kuchangia kiasi chochote cha fedha kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa hostel kutokana wanafunzi wa kike wanasoma katika mazingira sio rafiki.
“Vijana wetu wa kike wanakaa mtaani ambapo kuna changamoto nyingi ambazo zinawafanya wasifanye vizuri katika masomo yao, kuna vishawishi kama hawajawa makini wanaweza kupata maradhi kutokana na mazingira wanayoishi” amesema Mhe. Homera.
Rc Homera amesema kuwa wananchi wa Mkoa wa Mbeya wameanza safari ya kwenda kujenga hosteli za watoto wa kike ili kuhakikisha wanakaa katika mazingira rafiki.
“Nawapongeza Chuo Kikuu Mzumbe kwa kuja na wazo hili, mimi Mkuu wa Mkoa siweze kuwaacha nitahakikisha hosteli zinakamilika na watoto wa kike watapata hosteli za kisasa na kuishi katika mazingira mazuri” amesema Rc Homera.
RC Homera amewashukuru uongozi wa Chuo Kikuu Mzumbe, viongozi wa serikali, Wafanyabiasha, Vyuo vyote pamoja na wanafunzi kwa kuonesha ubunifu katika kufanikisha ujenzi wa hosteli unakamilika.
“Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson atakuja kutoa mchango wake, viongozi wa serikali wapo pamoja katika safari hii ili kuhakikisha malengo tarajiwa yanafanikiwa” amesema Rc Homera.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha, amesema kuwa lengo ni kuchangisha fedha kwa ajili ujenzi hosteli na kuwasaidia wanafunzi ili kuepukana na changamoto katika masomo yao.
Prof . Mwegoha amefafanua kuwa hatua hiyo ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais Mhe. Dkt. Samia Suruhu Hassani ambazo ameweka mwenyewe ili kuhakikisha miundombinu ya elimu inaimalika nchini.
Amesema kuwa Chuo kina wanafunzi wasichana 1, 724 sawa na asilimia 50.5 huku wavulana wakiwa 1,686 sawa na asilimia 49. 5.
Prof. Mwegoha ameeleza kuwa wasichana wanakutana na changamoto mbalimbali ikiwemo kutishiwa kubakwa pamoja na maradhi hivyo wameona ipo haja ya kuongeza miundombinu ili waweze kuishi karibu na eneo la Chuo.
“Tunakupongeza kwa kutuunga mkono jitihada za ujenzi wa hostel katika Chuo Chetu kwa lengo la kuboresha elimu kwa maendeleo ya Taifa letu” amesema Prof. Mwegoha
Ili kufikia lengo kwa wakati viongozi wa serikali, sekta binafsi, wadau wa maendeleo pamoja na wananchi kwa ujumla wanapaswa kushiriki harambee ya ujenzi wa hosteli kwa kuchangia kiasi chochote cha fedha kupitia control namba 994180331310.