Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini, Mhe. Cosato Chumi akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa iliyosomwa na Waziri Mhe. Innocent Bashungwa bungeni jijini Dodoma
“Narudia tena, wawezesheni Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wapeni miaka miwili tu, mtaona maajabu kama ya kule Chita, sio haki sisi kama Taifa kuagiza mchele kutoka nje, wezesheni JKT muone” – Mhe. Cosato Chumi, Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini
“Tumejionea kazi kubwa na nzuri ya ujenzi wa ikulu, vijana wa JKT wameshiriki, tuwawezeshe, tuwape miaka miwili, nawaambia tena hatutaagiza mafuta ya kupikia nje ya nchi” – Mhe. Cosato Chumi, Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini
“Ukimuona mwanajeshi mheshimu sana, usione tunaenda sokoni, kwenye ibada, tupo hapa Bungeni tunaendelea na vikao, ni kwa sababu wapo watu hawalali kwa ajili yetu, wanakesha kwa ajili ya ulinzi na usalama wetu” – Mhe. Cosato Chumi, Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini
“Kumekuwepo na nafasi haba za vijana wanaomaliza kidato cha sita wanakwenda JKT, pengine kwa kukosa uelewa tunaona kana kwamba JKT ndio wamewanyima nafasi vijana hao. Naomba Wizara ya Fedha iiwezezhe JKT ili vijana wengi waweze kujiunga” – Mhe. Cosato Chumi, Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini
“Nashauri hata watumishi wa umma wanaoajiriwa wapelekwe JKT hata mwezi mmoja tu, hakika tukifanya tutaona mabadiliko makubwa katika utendaji, tabia, uzalendo na mfumo mzima wa kufikiri” – Mhe. Cosato Chumi, Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini