Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uhamiaji Kenya, Prof. Julius Bitok (kushoto), kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kimataifa wa ID4AFRICA unaojadili masuala ya Ikolojia ya Utambuzi (Identity Ecosystem), unaofanyika jijini Nairobi nchini Kenya, leo Mei 23, 2023. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kaspar Mmuya.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Kaspar Mmuya (wapili kulia), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Vicent Kawawa (wapili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Mhandisi Ismail Rumatila, wakimsikiliza Mkuu wa Taasisi ya ID4AFRICA, Joseph Atick (hayupo pichani), alipokuwa anazungumza katika Mkutano wa Kimataifa ulioandaliwa na Taasisi hiyo, unaofanyika jijini Nairobi, nchini Kenya, leo Mei 23, 2023.
Mkuu wa Taasisi ya ID4AFRICA, Joseph Atick, akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa wa ulioandaliwa na Taasisi hiyo unaojadili masuala ya Ikolojia ya Utambuzi (Identity Ecosystem), unaofanyika jijini Nairobi nchini Kenya, leo Mei 23, 2023.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Kaspar Mmuya (watatu kushoto), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Vicent Kawawa (wapili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Mhandisi Ismail Rumatila (watatu kulia), wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kabla ya kuanza kwa Mkutano wa ID4AFRICA, unaofanyika jijini Nairobi, nchini Kenya, leo Mei 23, 2023.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia) akifurahi jambo wakati alipokuwa anazungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uhamiaji Kenya, Prof. Julius Bitok (kushoto), Kamishna wa Takwimu wa Uhamiaji nchini humo, Imaculate Kasait (wapili kushoto), pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kaspar Mmuya, kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kimataifa wa ID4AFRICA unaojadili masuala ya Ikolojia ya Utambuzi (Identity Ecosystem), unaofanyika jijini Nairobi nchini Kenya, leo Mei 23, 2023.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kaspar Mmuya (kulia), akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Vicent Kawawa kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kimataifa wa ID4AFRICA unaojadili masuala ya Ikolojia ya Utambuzi (Identity Ecosystem), unaofanyika jijini Nairobi nchini Kenya, leo Mei 23, 2023.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimtambulisha Katibu Mkuu wa Wizara yake, Kaspar Mmuya (wapili kushoto), kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uhamiaji Kenya, Prof. Julius Bitok (kulia), kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kimataifa wa ID4AFRICA unaojadili masuala ya Ikolojia ya Utambuzi (Identity Ecosystem), unaofanyika jijini Nairobi nchini Kenya, leo Mei 23, 2023. Wapili kulia ni Mkuu wa Taasisi ya ID4AFRICA, Joseph Atick.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Vicent Kawawa (kushoto), akimfafanulia jambo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Mhandisi Ismail Rumatila, kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kimataifa wa ID4AFRICA unaojadili masuala ya Ikolojia ya Utambuzi (Identity Ecosystem), unaofanyika jijini Nairobi nchini Kenya, leo Mei 23, 2023. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.