Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi vijana ajira na wenye ulemavu Patrobas Katambi akizungumza wakati akifunga maonesho hayo jijini Arusha.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi(NACTVET),Dk Adolf Rutayuga, akizungumza wakati wa kufunga Maonesho hayo jijini Arusha.
……
Julieth Laizer,Arusha.
Arusha.Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi vijana ajira na wenye ulemavu Patrobas Katambi amesema Mafunzo ya elimu ya ufundi na ufundi stadi ni muhimu katika kuandaa nguvu kazi yenye ujuzi inayohitajika hapa nchini na ina mchango mkubwa katika kutatua changamoto ya ajira kwa vijana.
Ameyasema hayo wakati akifunga maonesho ya elimu ya ufundi na Mafunzo ya ufundi stadi yaliyoanza mei 16 katika uwanja wa sheikh Amri Abeid Jijini Arusha
Amesema changamoto ya ajira inaweza kutatuliwa kwa kuwa na mipango madhubuti na mikakati endelevu ya kuwasaidia vijana kufika vyuoni na kupewa stadi zitakazo wasaidia kukuza ujuzi wa kutatua changamoto mbali mbali zinazolikabili Taifa.
“Nawaomba wadau wote wa Elimu ya ufundi na Mafunzo ya ufundi stadi kuendelea kushirikiana na serikali katika kuhakikisha kuwa Taifa linapata nguvu kazi yenye ujuzi na inayokidhi mahitaji ya Taifa.’amesema .
Kwa upande wake Katibu mtendaji baraza la taifa la elimu ya ufundi na Mafunzo ya ufundi stadi (NACTVET) Dk Adolf Rutayuga amesema kuwa,jumla ya Taasisi 145 zimeshiriki katika maonesho hayo ikiwemo Taasisi 98 ni vyuo vya ufundi na Mafunzo ya ufundi stadi , Taasisi 11 ni vyuo vikuu , Taasisi 30 ni kampuni zilizofanikiwa kupitia elimu ya Mafunzo ufundistadi huku Taasisi sita zikiwa ni makampuni za biashara na Mamlaka za udhibiti.
Akizungumza kwa niaba ya chuo Cha mipango kilichoshiriki katika maonyesho hayo,Naibu Mkurugenzi taaluma amesema kuwa, Maonesho hayo yameleta mafanikio makubwa sana ambapo wananchi mbalimbali wamepata fursa ya kujifunza kuhusu maswala mbalimbali.
Maonesho hayo yaliandaliwa kwa ushirikianao wa NACTVET na Taasisi za vyuo vya elimu ya ufundi na Mafunzo, Chama cha waajiri Tanzania ATE , sekretariet ya mkoa wa Arusha , Wadau mbali mbali wa Elimu ufundi na Mafunzo ya ufundi stadi huku kauli mbiu ikiwa ni “elimu ya ufundi na Mafunzo ya ufundi stadi kwa nguvu kazi mahiri”.