IIle dhana ya wananchi wanaoishi pembezoni mwa migodi ni watu masikini na wa kutupwa sasa inakwenda kuondoka kutokana na mfumo mpya ulioanzishwa na Mgodi wa Barrick North Mara kuwainua kiuchumi wananchi.
Hali hiyo inatokana na mgodi huo kuja na mpango wa uwezeshwaji wananchi kiuchumi kupitia kilimo biashara ambapo wameanzisha shamba lenye ekari 10 kwa ajili ya vikundi vya kijamii katika vijiji 11 vinavyozunguka mgodi wa Barrick North Mara.
Akizungumza katika shamba hilo, mtaalamu wa Kilimo kutoka mgodi wa Barrick North Mara, Praygod Mushi alisema shamba hilo ni mpango wa mgodi huo kubadilisha mtazamo wa wananchi kuhusiana na uchumi na ndio maana wameanza na kilimo.