Kutoka Dodoma 22/5/2023
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MMM Group kutoka nchi ya Ujerumani iliyojikita kwenye masuala ya ujenzi wa miundombinu Bw. Peter Mäsgen, ili kujadili kuhusu fursa mbalimbali za uboreshaji miundombinu katika Sekta ya afya nchini.
Dkt. Mollel ameipongeza Kampuni hiyo kwa kuonesha nia ya kuja kuwekeza nchini katika Sekta ya Afya, huku akiwakaribisha wawekezaji mbalimbali kuja nchini kwani Serikali ya Rais Samia imeweka mazingira mazuri kwa wawekezaji kutoka nje na ndani ya nchi.
“Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya uwekezaji mkubwa wa miundombinu ya kutolea huduma za afya nchini, lakini bado tunahitaji zaidi wawekezaji kama hawa wanaokuja na teknolojia mpya zitakazowezesha usogezaji wa huduma za afya karibu zaidi kwa wananchi, Serikali kupitia Wizara ya Afya tunawakaribisha wawekezaji na tutawapa ushirikiano wa kutosha.” amesema Dkt. Mollel.
Kwa upande wake Mkurugeni Mtendaji wa MMM Group Bw. Peter Mäsgen amesema kuwa, kampuni yake imejikita kwenye masuala ya ujenzi wa miundombinu kwa kutumia Teknolojia za kisasa na hutumia muda mfupi kukamilisha ujenzi wa majengo na vifaa vyake.
Mkurugeni Mtendaji wa MMM Group Bw. Peter Mäsgen