Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohamed (katikati) akisisitiza jambo kwa mnufaika wa Mafunzo ya Ujuzi sekta ya Utalii alipotembelea banda la TEA kwenye maonesho ya Elimu ya Ufundi yanayoendelea viwanja vya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati,Anna Mbogo (kushoto) pamoja na wamama wajasiriamali wa Mkoa wa Arusha wakifurahia bidhaa za utalii wa kitamaduni kutoka kwa mnufaika wa mafunzo ya Kuendeleza Ujuzi (SDF) katika maonesho ya Elimu ya Ufundi yanayofanyika Jijini Arusha viwanja vya Sheikh Amri Abeid
Lyidia Mathias Mnufaika wa Mafunzo ya Ujuzi katika Sekta ya Utalii wl LLa kitamaduni akitoa elimu kwa mdau wa masuala ya utalii aliyetembelea banda la TEA kwenye maonesho ya Elimu ya Ufundi yanayoendelea Jijini Arusha .
…………………………..
Julieth Laizer ,Arusha.
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imefadhili vijana 600 kutoka Zanzibar kupitia Mfuko wa kuendeleza ujuzi (SDF) wa kusaidia vijana kupata mafunzo ya ujuzi.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi idara ya utafutaji Rasilimali na usimamizi wa miradi TEA,Masozi Nyiremba wakati Waziri wa elimu na mafunzo ya Amali Zanzibar ,Lela Mohamed alipotembelea banda hilo katika maonesho ya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi katika viwanja vya stadium jijini Arusha.
Nyirenda amesema kuwa ,vijana hao 600 walionufaika na mfuko huo ni kutoka kaya maskini na waliosajiliwa na Mfuko wa Tasaf ambapo wamekuwa wakifadhiliwa ada za mafunzo ,usafiri ,Malazi na chakula na kila mmoja anasomea kozi mbalimbali.
Amesema kuwa ,programu hiyo ilianza desemba mwaka jana ambapo lengo kuu la mfuko huo ni kuwezesha Taasisi zinazotoa mafunzo kuongeza ubora na ufanisi katika kutoa mafunzo ya ujuzi na stadi za kazi katika sekta sita za kipaumbele nchini.
“Mfuko wa SDF ni sehemu ya Programu ya kuendeleza Elimu ya ujuzi na mafunzo ya stadi za kazi zenye kuleta tija katika ajira na mpango mkakati wa kitaifa wa kukuza na kuendeleza ujuzi nchini “amesema.
Aidha amefafanua kuwa,mfuko unasimamiwa na Mamlaka ya elimu Tanzania (TEA) na unapata ufadhili kutoka Benki ya Dunia na serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa upande wake Waziri wa elimu na mafunzo ya Amali Zanzibar Lela Mohamed Mussa alipongeza mamlaka hiyo kwa ufadhili huo kwani umesaidia kwa kiwango kikubwa kutatua changamoto ya ajira kwani tayari vijana wengine walishajiajiri tayari.
Aidha ametoa rai kwa Wadau mbalimbali kuangalia namna ya kuwapatia mikopo vijana hao ambao tayari wameshapewa ujuzi na mfuko huo ili waweze kuendeleza shughuli zao na kuweza kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande wa binti wa kiasi aliyenufaika na mfuko huo,Lydia Mathias(20) mkazi Mto wa mbu amesema kuwa, kabla ya kupata fursa hiyo kutoka mfuko huo alikuwa akiishi maisha magumu kutokana na kushindwa kuendelea na kidato cha pili kutokana na ukosefu wa mahitaji y shule huku akilazimishwa kuolewa akiwa umri mdogo.”
“Mimi niliona matangazo kuhusu ruzuku hiyo inayotolewa na mfuko huko ndio nikaomba na mimi namshukuru Mungu nilipata nikasoma miezi mitatu nikipata ujuzi wa kitaaluma kuhusu kutengeneza bidhaa za asili ikiwemo shanga,na vitu mbalimbali na sasa hivi imeweza kuanzisha kikundi changu kinaitwa Naserian na nimeajiri watu 50 tayari.