Mbunge wa Jimbo la Ilala ambaye pia Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Zungu akizungumza na wachezaji wa timu ya Mnazi mmoja na Mtambani A kabla ya mchezo wa fainaili wa Wazazi Cup Kata ya Jangwani kuanza katika Viwanja vya JK Park Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala Bw. Said Sidde akisalimia na wachezaji wa mpira wa miguu katika mashindano ya Wazazi Cup Kata ya Jangwani Viwanja vya JK Park Jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Kamati ya Michezo Chama Cha CCM Wilaya ya Ilala, Pia Mwenyekiti wa Mashindano Kata ya Jangwani Bw. Imran N. Jaffer maarufu kwa jina la Imran Baba (kushoto) akipokea Cheti Cha Shukurani kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya wa Wazazi Kata ya Jangwani Bw. Ally Sindo baada ya kuwezesha mashindano ya Wazazi Cup Kata ya Jangwani kufanikiwa.
Katibu wa CCM Kata ya Jangwani
Bi. Riziki Kisingiti akitoa zawadi kwa mshindi wa kwanza timu ya Mnazi mmoja katika mashindano ya Wazazi Cup Kata ya Jangwani katika Viwanja vya JK Park Jijini Dar es Salaam.
Viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala wakiwa katika picha ya pamoja na Mabigwa wa Mashindano ya Wazazi Cup Kata ya Jangwani Mnazi mmoja.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Ilala Sabbry Sharif (kulia) akizungumza jambo na Mjumbe wa Kamati ya Michezo Chama Cha CCM Wilaya ya Ilala, Pia Mwenyekiti wa Mashindano Kata ya Jangwani Bw. Imran N. Jaffer maarufu kwa Jina la Imran Baba wakati wakitazama mchezo wa fainaili Wazazi Cup Kata ya Jangwani uliofanyika Viwanja vya JK Park Jijini Dar es Salaam.
…..
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Mashindano Ya Wazazi Cup Kata Ya Jangwani yamefikia tamati baada ya timu ya Mnazi mmoja kuifunga Mtambani A kwa changamoto ya mikwaju ya penati katika mchezo wa fainali uliochezwa leo tarehe 20/5/2023 katika Viwanja vya JK Park Jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo wa fainali viongozi kutoka mbalimbali wameshiriki akiwemo Mbunge wa Jimbo la Ilala ambaye pia Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Zungu, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala Bw. Said Sidde, Madiwani pamoja na viongozi wa CCM ngazi ya Kata na Matawi.
Mhe. Zungu amesema kuwa ataendelea kutoa ushirikiano katika kuhakikisha michezo inasonga mbele pamoja kuandaa mishindano katika Jimbo la Ilala.
“Katika mashindano ya Wazazi Cup Kata ya Jangwani leo natoa Sh. 200,000 kwa ajili ya kuongezea zawadi, pia nawapongeza kwa kuandaa mashindano haya” amesema Mhe. Zungu.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala Bw. Said Sidde amewataka vijana kuwa na nidhamu pamoja kuwa na utamaduni wa kushiriki michezo mara kwa mara.
Mjumbe wa Kamati ya Michezo Chama Cha CCM Wilaya ya Ilala, Pia Mwenyekiti wa Mashindano Kata ya Jangwani Bw. Imran N. Jaffer maarufu kwa jina la Imran Baba, amesema kuwa lengo ni kuwasaidia vijana, hivyo kama mdau wa michezo ataendelea kutoa ushirikiano ili kuhakikisha malengo tarajiwa yanafikiwa.
“Katika Kata ya Jangwani tutakuwa tunaandaa michezo ya aina mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, netball na basketball” amesema Imran Baba.
Amesema kuwa ukishiriki michezo ina faida kiafya hivyo ni vizuri mtu akafanya mazoezi mara kwa mara kwani ni njia bora ya kuwa fiti kimwili pamoja na afya njema ya kisaikolojia.
“Watu wakishiriki michezo akili yao inafanya kazi vizuri tofauti na ukikaa bila kufanya mazoezi yoyote, kutokana na umuhimu wa michezo nitahakikisha katika Kata ya Jangwani inafanyika kila baada ya miezi mitatu, pia tutaweka na michezo ya wanawake ili nao waweze kushiriki” amesema Imran Baba.
Amefafanua kuwa jumuiya ya wazazi ina uwajibu wa kuwalea vijana ili wawe na maadili mema kwa kuandaa programu za michezo kwa ajili ya kuwaelimisha ili kuwaepusha vishawishi ikiwemo kutumia dawa za kulevya.
“Natoa wito kwa wadau mbalimbali kuonesha ushirikiano wa kusaidia kufanikisha mipango ya utekelezaji wa kuandaa programu za michezo” amesema Imran Baba.
Katibu wa CCM Kata ya Jangwani
Bi. Riziki Kisingiti ameipongeza kamati ya mashindano ya Wazazi Cup kwa kuandaa na kufanikiwa.
“Tunamshukuru Imran Baba kwa kuwezesha mashindano ya Wazazi Cup Kata ya Jangwani hadi kufikia tamati na kupatikana mshindi” amesema Bi. Kisingiti.
Ameeleza kuwa kila kitu kimekwenda sawa, huku akieleza kuwa mshindi wa kwanza ni timu ya Mnazi mmoja ambayo imepata zawadi Sh. 400,000 pamoja na mipira miwili.
Mshindi wa pili timu ya Mtambani A ambapo imepata zawadi ya Sh. 200,000 pamoja mpira mmoja, huku mshindi wa tatu akipata Sh 100,000.
Bi. Kisingiti amewataka wazazi kutoa ruhusu kwa vijana wao kushiriki michezo kwa ajili ya kuunga juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suruhu Hassani katika kuendelea michezo.
Mwenyekiti wa Jumuiya wa Wazazi Kata ya Jangwani Bw. Ally Sindo, amesema kuwa mashindano hayo ni sehemu ya maandalizi ya kuandaa timu kwa ajili ya kushiriki Mashindano ya Wazazi Super Cup ngazi ya Mkoa.
Katika fainali hizo viongozi wa Jumuiya ya wazazi kutoka kata mbalimbali Wilaya ya Ilala wameshiriki akiwemo Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Kata ya Ilala Sabbry Sharif na kutoa pongezi kwa waandaaji wa mashindano kwani ni jambo rafiki katika kuhakikisha inapatikana timu bora inayokwenda kushiriki mashindano ya wazazi Super Cup ngazi ya Mkoa.